Wednesday, January 2, 2013

MASTAA WAPOKEA TAARIFA YA KIFO CHA SAJUKI KWA HUZUNI KUBWA




Baada ya kuugua kwa muda mrefu, hatimaye aliyekuwa muigizaji wa filamu nchini, Juma Kilowoko maarufu kama Sajuki amefariki dunia leo alfajiri katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa Katibu wa chama cha waongoza Filamu Wilaya ya Ilala, Rajabu Amiri hivi karibuni Sajuki alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu,mgongo na kansa ya ngozi

Sajuki alikuwa akitakiwa kurejea tena nchini India kwaajili ya kuendelea na matibabu ya tatizo lililokuwa likimsumbua ambapo jumla ya shilingi milioni 28 zilikuwa zikihitajika.

Hivi karibuni ilidaiwa kuwa alikuwa ameshakusanya shilingi milioni saba tu zilizotokana na michango ya watu na show alizokuwa akizifanya kukusanya fedha hizo. Show ya mwisho aliifanya jijini Arusha ambako alianguka kwenye stage.

Kifo hicho cha Sajuki kimepokelewa kwa masikitiko makubwa kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo mastaa wa Tanzania waliotumia mitandao ya kijamii kuelezea masikitiko yao.

Mwasiti Almas
Tunapolala na kuamka tunasema AHSANTE kwa mungu,tunapopoteza pia tunaowapenda tuseme AHSANTE… alichokileta ALLAH chini ya jua atakichukua

Salama A. Jabir
Mwenyezi Mungu Akusamehe Makosa Yako Ndugu Yetu Juma Kilowoko..Ucheshi Wako Ntaukumbuka Milele. Pumzika Kwa Amani Rafiki. #RIPSajuki

Jokate Mwegelo
Nimesikia hii habari sasa. Sad lakini kazi ya Mungu haina makosa tunazidi kumtumainia yeye na kumshukuru. Upumzike kwa amani sajuki. Amen!!

Zitto Zuberi Kabwe
Hali ya Afya ya Sajuki ndiyo ilinisukuma sana kuanza kusaidia wasanii nchini kupata kipato stahili na kazi Yao. Kifo chake kimeniondolea Mtu niliyemtazama kama kishawishi Cha Mimi kupigania haki za Watanzania walio kwenye entertainment industry. Sajuki left an indelible mark in my politics. Pumzika Kwa Amani Juma.

Masanja ‏Mkandamizaji
Duniani si nyumbani kwetu. Ni njia tu.

Hemedy Suleiman
R.I.P SAJUKI……..daaaaaah this is painful!!

Arnold Kayanda
Pamoja na kuwa Msiba wowote unanisikitisha ila wa Sajuki unanisikitisha zaidi kila napoikumbuka Historia yake na Mkewe!

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...