

Alisema kuwa Black Leopards ni timu nzuri na walipata mazoezi mazuri katika mechi ya kwanza iliyofanyika kwenye uwanja waTaifa jijini na kushinda kwa mabao 3-2.
“Ni mechi nzuri ambayo nadhani itakuwa ni kipimo kikubwa kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, wachezaji wangu wana viwango vizuri sana kwa sasa na naamini makosa yaliyofanyika katika mechi ya kwanza hawatayafanya tena,” alisema Brandts.
Msemaji wa Klabu Yanga, Baraka Kizuguto alisema jana kuwa pamoja na mechi hiyo kuwa ya maandalizi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, pia wameamua kuicheza ili kuwapa burudani mashabiki wa Mwanza.
Kizuguto alisema kuwa Yanga haitakuwa na mechi yoyote katika mzunguko wa pili Kanda ya ziwa na hiyo ndiyo nafasi yao ya kuwaonesha uwezo wao mkubwa mashabiki wa Mwanza nini wamekipata kutoka Uturuki.
“Tuna mashabiki wengi sana Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla, hii ni fursa kwetu kwani mahsbaiki na wanachama watapata fursa ya kuona kiwango na maandalizi ya timu yao kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili,” alisema Kizuguto.
No comments:
Post a Comment