SHIRIKISHO la Filamu Tanzania (TAFF) limekemea baadhi ya wasanii walioonyesha utovu wa nidhamu katika msiba wa aliyekuwa msanii wa filamu nchini, Juma Kilowoko ‘Sajuki’.
Pia limesisitiza kuwa msanii atakaeripotiwa katika vyombo vya habari kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu atafungiwa kuigiza.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Rais wa TAFF, Simon Mwakifwamba alisema amesikitishwa na kitendo cha wasanii kuacha msiba na kwenda kunywa pombe wakati msiba huo ni wa dini inayopinga unywaji wa pombe.
Alisema baadhi ya wasanii kuonyesha utovu wa nidhamu katika msiba wa marehemu Kanumba na wengine katika msiba wa Sajuki.
“Nasikitika kuona msanii hajitambui hata kidogo, yani anaacha msiba anakwenda kunywa pombe tena jirani na mahala pa msiba, jamani huu msiba ni wa dini, hivyo atakayeripotiwa vibaya katika misiba TAFF tutamfungia” alisema Mwakifwamba.
Katika hatua nyingine alisema msiba huo ulitawaliwa na utani hali ya kwamba umewakutanisha watani wa makabila.
Msiba huo ulitawaliwa na utani baada ya kuwepo kwa wasanii wachekeshaji kama vile, Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya fedha, Lucas Mhuvile ‘Joti’ na wengineo wengi.
No comments:
Post a Comment