Thursday, January 3, 2013

AIRTEL YAWAZAWADIA WASHINDI WA MWEZI WA PROMOSHENI "AMKA MILIONEA" SHILINGI MILIONI 30‏

Meneja Bidhaa wa Airtel, Francis Ndikumwami (wa pili kushoto) na Mwakilishi wa Bodi ya Bahati Nasibu ya Taifa, bw Sadiki Elimsu (wa kwanza kushoto) wakitafuta washindi wa mwezi wa promosheni ya Amka Milionea ambapo mmoja kati ya washindi ni Bw. Rickson Richard kutoka Arusha ambaye amejishindia kitita cha shilingi milioni 15. Wanaoshuhudia ni waandishi wa habari, kulia ni Afisa Uhusiano wa Airtel, Bi. Jane Matinde. 
 · Washindi wawili wapatikana, Kila mmoja aondoka na kitita cha shilingi milioni 15
Januari 2, 2013 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayotoa huduma nafuu na yenye wigo mpana zaidi wa mawasiliano, leo iwatangaza washindi wa mwenzi wa promosheni “Amka Millionea” wa pesa taslimu million 30 mara baada ya kuibuka washindi kupitia droo iliyofanyika leo asubuhi ambapo kila moja ameibuka na kitita cha shilingi milioni 15 pesa taslimu.
Akitangaza washindi hao mara baada ya droo iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde alisema” Airtel inawapa nafasi nyingine watanzania kushiriki na Kushinda fedha taslimu kwa kupiti promosheni yetu hii kabambe ya “Amka Millionea” iliyozinduliwa mwanzoni mwa mwenzi December, mpaka sasa wateja zaidi ya 300 wamejishindia zawadi za pesa taslimu zenye thamani zaidi ya shilingi million 120. Promosheni ya Amka millionea inawazawadia wateja wa Airtel Kila siku , kila wiki na leo tunashuhudia wateja wawili wa mwisho wa mwenzi wakiibuka kuwa washindi wa shilingi million kumi na tano kila mmoja.
Tunaendelea kuwajali na kuwazawadia wateja wetu nchi nzima kuhakikisha washindi wengi wanapatikana, tunaendelea kuimarisha dhamira yetu ya kutoa huduma bora zenye viwango vya juu na kudhihirisha kauli mbiu yetu ya jisikie huru, aliongeza Matinde
Akiongea kwanjia ya simu mara baada ya kutangazwa mshindi, Rickson Richard mkazi wa Arusha na mwanafunzi wa kidato cha tano katika shule ya Lyamungo high school alisema’ nimefurahi kuibuka mshindi wa milioni 15 wa promosheni ya Amka millionea, pesa hizi ntazitumia katika masomo yangu shule na kumsaidia baba yangu ambaye ndiye aliyenipa pesa za kuchezea promosheni hii. nawaambia watanzania ­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­waamini wanaweza kushinda na kujiunga kwani mimi nimecheza na nimeshinda kwa Bahati nao pia wananafasi ya kujishindia kama mimi.
Tunapenda kuwajulisha kuwa promosheni hii bado inaendelea na kukupa nafasi ya kuwa mmoja kati ya washindi wa mamilioni ya fedha kila siku, kila wiki, kila mwezi au mshinid wa zawadi kubwa moja itatolewa mwisho wa promosheni.
Ili mteja aweze kushiriki inabidi atume neno WIN/SHINDA kwenda namba 15595 bure , Baada kujiunga mteja atakuwa atapata ujumbe kutoka 15656 na kupata maswali ambayo atajibu na akipata sahihi atapata ponti 20 akikosea atapata ponti 10. Na kwakila ujumbe atakaotuma atatozwa kiasi cha shilingi 350 pamoja na kodi.
Afisa Uhusiano wa Airtel, Bi Jane Matinde akiongea na mshindi wa Amka Milionea, Bw. Rickson Richard (19) kutoka Arusha mara baada ya kuibuka mshindi wa shilingi milioni 15 wa promosheni ya Amka milionea, Katikati ni Meneja Bidhaa Francis Ndikumwami akifuatiwa na Mwakilishi wa Bodi ya Bahati Nasibu ya Taifa, Bw. Sadiki Elimsu.

Afisa Uhusiano wa Airtel, Bi. Jane Matinde akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuendesha droo ya mwezi ya washindi wa Amka Milionea, ambapo mmoja kati ya washindi ni Bw. Rickson Richard kutoka Arusha aliyejishindia shilingi milioni 15. Pichani Katikati ni Meneja Bidhaa Francis Ndikumwami akifuatiwa na Mwakilishi wa Bodi ya Bahati Nasibu ya Taifa, Bw. Sadiki Elimsu.




No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...