Tuesday, December 11, 2012

RAYC amtembelea Rais Kikwete Ikulu jijini Dar, amshukuru kwa msaada wa matibabu.


RAY C akimshukuru Rais Kikwete kwa matibabu Ikulu jijini Dar es Salaam jana. 
 
Msanii wa Kizazi Kipya hapa nchini ,maarufu kama Bongo Flavour, Bi Rehema Chalamila anmeaejulikana zaidi kama Ray C,jana mchana alifika Ikulu ya Dar-Es-Salaam kumshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa msaada mkubwa wa matibabu yake ambayo yanafanyika jijini Dar-Es-Salaam chini ya uangalizi maalum

Ray C amefika Ikulu akiongozana na mama yake mzazi Bibi Margareth Mtweve ambaye pia alishukuru Rais Kikwete kwa msaada huo mkubwa ambao umesaidia kurudisha hali ya kawaida ya Ray C.

Rais amempongeza Ray C kwa kukubali hali yake ya kiafya na hatimaye kukubali kupata matibabu ambayo bado anaendelea nayo chini ya uangalizi maalum.

Rais alimtaka mwanamuziki huyo kufuata masharti ya madaktari ili aweze kupona kabisa na hatimaye kurudia hali yake ya mwanzo na kurejea katika shughuli zake za kujitafutia kipato na maisha.

Kwa vile Ray C bado yuko katika matibabu, hatutaweka wazi sehemu anayotibiwa hadi atakapokuwa tayari kabisa kurudi katika shughuli zake rasmi hivyo tunaomba jamii impe ushirikiano huo na kuheshimu taratibu zake za matibabu ili hatimaye aweze kupona kikamilifu.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Ray C watatu kushoto,Mama yake mzazi RayC Bibi Margareth Mtweve (kushoto) na kulia ni Sarah Mtweve Dada yake Ray C. (picha

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...