Tuesday, November 6, 2012

RAIS KIKWETE ATOA POLE KWA KATIBU ALIEMWAGIWA TINDIKALI


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali na kumpa pole Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhili Soraga ambaye amelazwa katika chumba cha dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufuatia majeraha ya usoni na kifuani yaliyotokana na kurushiwa Tindikali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazoezi katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe mjini Unguja juzi. Rais ambaye amerejea Jana Jumanne Novemba 6, 2012 akitokea katika ziara ya kikazi ya takriban juma moja katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Singida, amemtakia Sheikh Soraga nafuu ya haraka.


No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...