MShiriki wa Redds Miss Tanzania 2012, Babylove Kalala akijarimu kumuuma nyoka wakati mrembo huyo pamoja na wenzake wanaowania taji hilo walipotembelea eneo la Snake Park mjini Arusha.
Warembo wanaowania taji la Redds Miss Tanzania 2012 jana walitembelea eneo la Utalii la ufugaji nyoka la mjini Arusha maarufu ARUSHA SNAKE PARK na kujionea nyoka wa aina mbalimbali, Mamba, Kenge, ndege aina ya Bundi, Tai na Tumbiri.
Warembo hao wapo Mikoa ya Kanda ya Kaskazini kwaajili ya kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii nchini na kujifunza mambo tofauti tofauti.
Pamopja na kujionea Nyoka hao na kucheza nao kwa kuwa vaa shingoni pia warembo hao walipata fursa ya kujifunza juu ya tamaduni za Mila ya Wamaasai na kutembelea vibanda vya urembo wa Kimasai.
Mrembo wa Kilimanjaro, Anande Raphael (kushoto) akipozi na Mrembo wa Lindi, Irine Veda huku wakiwa na nyoka.
Mrembo Diana Hussein nae aliweka mapozi yake na nyoka
Warembo wakimwangalia Catherine Masumbigana aliyemzungusha nyoka shingoni
Hapa ni Mrembo wa Kitongoji cha Ukonga jijini Dar es Salaam, Mary Chizi akila pozi.
Jesca Haule mrembo kutoka Kitongoji cha Chang'ombe jijini Dar es Salaam nae alionesha ujasiri wake wa kumvaa nyoka.
Wapo walio ogopa kama Miss Photogenic 2012, Lucy Stephano
Mrembo wa Mbeya Caren Elias nae aliogopa sana. Kulia ni Noela Michael kutoka Tabata nae akiogopa hata nyoka hajamshika.
Lightness Michael nae aliweka pozi na Nyoka
Fina Revocatus kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha akipozi na wenzake.
Warembo wakiwa katika eneo la Historia ya Jamii ya wamaasai ambayo nayo ipo Meserani mjini Arusha.
Mrembo wa Pwani, Rose Lucas akipita katika sehemu ya Historia ya Wamasai.
Miss Tanzania 2011, Salha Izrael nae akitoka katika vibanda vya biashara
Elizabeth Diamond mrembo kutoka Singida akiangalia shanga na urembo za aina mbalimbali kwaajili ya kununua.
Mrembo wa Kahama Mkoani Shinyanga, Happiness Rweyemamu nae alikuwa akitafuta cha kununua.
Mkuu wa Itifaki ya Miss Tanzania, Albert Makoye akipiga picha na warembo wa
Miss Tanzania akiwa amevalia vazi rasmi la Kabila la Kimasai.
Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania, Albert Makoye na Mrembo Joyce Baluhi wakiwa wamevalia mavazi rasmi ya jamii ya Wamaasai.
No comments:
Post a Comment