Thursday, October 11, 2012

BABY MADAHA AFIWA NA MAMA YAKE

 
Msanii wa filamu na muziki wa kizazi kipya bongo Baby Madaha, yupo katika huzuni kubwa baada ya kumpoteza mama yake mazazi juzi usiku baada ya kuumwa kwa muda mrefu. Mwili wa marehemu umesafirishwa jana kupelekwa Musoma nyumbani kwao ambapo mipango yote na taratibu za kuzika zitajulikana huko.

Mwandishi wa habari hizi alifika kwenye msiba huo maeneo ya Kinondoni, na kukutana kuna umati mkubwa wa watu ambao walifulika kumpa pole msanii huyo ambaye ni kipenzi cha watu.

Hata hivyo mwandishi wa habari hizi, alizungumza na Madaha ingawa hakuweza kuzungumza sana zaidi ya kutokwa machozi huku akisema kuwa amempoteza mama yake kipenzi ambaye alikuwa akimsapoti kwenye vitu vingi ndani ya maisha yake.

“Naumia sana lakini najua yote ni mipango ya Mungu kwani kila kitu kimepangwa, hivyo tunamuombea mama yetu aweze kwenda salama mbele za haki kwani sote hiyo ndiyo njia yetu,” alisema kwa maskitiko

1 comment:

  1. Pole dada kwa kufiwa mama mupenzi kwa watu wote mungu amuwepe mahaka pema.

    ReplyDelete

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...