Tuesday, September 18, 2012

WEMA SEPETU ACHAFUA HALI YA HEWA MORO.


Wema Sepetu

Mwanadada anayefanya vyema katika kasnia ya filamu bongo, Wema Sepetu juzi alijikuta akiwaacha watu midomo wazi katika tamasha la Serengeti Fiesta katika Mji wa Morogoro baada ya kupanda jukwaani na kivazi kulichoshindwa kuyasitiri maungo yake nyeti na kuyaacha wazi.
Hivi kweli ni vituko vya mastaa wa kibongo hasa hawa wa Bongo Movie. Najiuliza sipati jibu hii ni kutokana na nini? Maana sijawahi kuona mastaa Kenya au Uganda wakifanya hivi sijui hawa wetu hawajitambui au inakuweje,sasa kwa namna hii tuseme ndio kioo cha jamii? La! Huku ni kujishushia heshima.
Mabadiliko ya kina yanahitajika vinginevyo tutaifanya hii sanaa ishindwe kusonga mbele na jamii kuichukulia kama ni ya kihuni.


No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...