Monday, September 3, 2012

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA NDANI YA UWANJA WA CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA


Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti kutoka Clouds Media Group Bwa. Ruge Mutahaba akisoma namba ya mshindi aliyejishindia gari aina ya Vits ambazo zimekuwa zikitolewa na kampuni ya Push Mobile katika mchakato mzima wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2012,Kati ni Meneja Masoko wa kampuni ya Push Mobile Bwa,Rugambo Rodney na shoto ni mmoja wa wakilishi wa bodi ya Taifa ya michezo ya kubahatisha Bwa.Bakari Maggid wakishuhutia tukio hilo usiku huu ndani ya uwanja wa CCM Kirumba.Mshindi wa gari hiyo aina ya Vitz alitajwa kuwa ni Bahati Joseph,mkazi wa jiji la Mwanza,mjasilia mali.

Baadhi ya mashabiki wakiwa wamejitokeza usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,linalofanyika kwenye uwanja wa ccm Kirumba.

Msanii wa bongofleva,Bob Junior a.k.a Shombe shombe akitumuiza na densa wake jukwaani

Pichani kulia ni msanii Recho kutoka THT akiwa sambamba na densa wake wakionesha umahiri wa kuimba jukwaani mauno kwa mbalii hivi.

Sehemu ya timu ya amsha amsha ya tamasha la serengeti fiesta 2012,kulia ni Dj Fetty,Bonge,Mully

Msanii wa kike anaekuja kwa kasi Recho akiimba kwa hisia jukwaani usiku huu

Sehemu ya umati wa watu ukishangweka vilivyo usiku huu ndani ya uwanja wa ccm kirumba.

Msanii wa hip hop Roma Mkatoliki akiwa amepozi na mashabiki wake kabla ya kupanda jukwaani usiku huu.

Msanii Ney wa Mitego kama kawa akikamua kwa hisia mbele ya wakazi wa jiji la Mwanza (hawapo pichani) waliojitokeza kwa wingi ndani ya uwanja wa ccm kirumba.

Msanii Ommy Dimpoz pozi kwa pozi akitumbuiza jukwaani na kundi lake.

Mwanadada machachari kabisa awapo jukwaani,Mwasiti akiimba jukwaani usiku huu.

Mzee wa Miduara katika anga ya muziki wa kizazi kipya,IT akiimba jukwaani.

Masharobaro ndio habari ya mujiniiiii....! Bob Junior na kundi lake wakitumbuiza kwenye jukwaa la Serengeti fiesta 2012 usiku huu kwenye uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza.

Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya aka Bongofleva, Prof Jay akishusha mistari yake kama kawa mbele ya umati wa watu (hawapo pichani),usiku huu ndani ya uwanja wa CCM Kirumba.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...