Monday, September 3, 2012

MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI AFARIKI DUNIA KWENYE VURUGU ZA BAINA YA WAFUASI WA CHADEMA NA POLISI KATIKA KIJIJI CHA NYOLOLO, MUFINDI IRINGA


Daudi Mwangosi
  Daud Mwangosi ameuwawa jana katika vurugu za Polisi na wafuasi wa CHADEMA katika kijiji cha Nyololo, Mufindi, Iringa.

Mwangosi aliuawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za CHADEMA Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi.

Kabla ya kuuawa kwa mwanahabari huyo, mabomu yalipigwa eneo hilo ili kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa hawapo tayari kuondoka katika ofisi yao.

Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuawa kilitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa, Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo kutaka kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kichapo na baadaye mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na askari mmoja waliaguka chini.

Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti.

Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa CHADEMA kurushiana mawe kwa mabomu, zaidi ya magari matano ya CHADEMA na ya wananchi yameharibiwa, huku watu kadhaa wakiachwa wamejeruhiwa hali mwanahabari mmoja, Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya. 

  
Marehemu Daud Mwangosi (kulia) akiwa kazini dakika 20 kabla ya mauti kumfika.
 
Mwandosi akiwa katikati ya polisi kabla ya kifo chake.



No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...