Wednesday, September 26, 2012

KAMATI YA UCHAGUZI TFF YATUPA RUFANI YA WARUFANI IRFA



Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana jana (Septemba 25 mwaka huu) kusikiliza rufani iliyowasilishwa mbele yake na warufani Mussa H. Mahundi, Abou O. Sillia na Alex Mgongolwa dhidi ya Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Iringa (IRFA) iliyoomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa IRFA uliofanyika Septemba 8 mwaka huu Mufindi, Iringa, na kuomba uchaguzi huo ufanyike upya kwa kuendeshwa na kusimamiwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF.


Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Deogratias Lyatto, baada ya kupitia maelezo ya warufani na warufaniwa, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imejiridhisha kuwa rufani iliyowasilishwa mbele yake na Mahundi, Sillia na Mgongolwa ilikosa sifa ya kuwa rufani kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF, Ibara ya 8(2), Ibara ya 21(3) na 24(2). Kwa kutozingatia matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imetupa rufani hiyo.


Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeiagiza Kamati ya Uchaguzi ya IRFA kuchukua hatua dhidi ya Abuu Changawa kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF, Ibara ya 28(6) kwa kuin

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...