Wednesday, September 19, 2012

AIRTEL YAPEWA CHETI CHA HESHIMA KWA KUWA WADAU WAZURI WA USALAMA BARABARANI

Meneja wa Nyanda za Juu Kusini wa Airtel Tanzania, B. Beda Kinunda akipokea cheti cha heshima toka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Dk. Emmanuel John Nchimbi wakati wa ufunguzi rasmi wa maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani mkoani Iringa kwa ajili ya kuhamasisha jamii kuzingatia sheria barabarani katika viwanja vya Samora mkoani hap


Maadhimisho ya wiki ya Usalama Barabarani yamefanyika rasmi mkoani Iringa huku maandamano maalum kwa ajili ya kuhamasisha jamii kuzingatia sheria barabarani yakifanyika katika viwanja vya Samora mkoani hapo.
Katika maadhimisho hayo kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ilikabidhiwa cheti cha kushiriki na kuwa wadau wazuri wa usalama barabarani.
Akiongea katika maadhimisho hayo Katibu Mwenezi wa Usalama barabarani, Bw. Heri Bantu ameyataka makampuni na taasisi mbalimbali kuiga mfano wa kampuni ya Airtel kwa kutoa mchango wa hali na mali katika kupunguza ajali barabarani. Aidha amewataka wananchi wote kuwa makini kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Usalama Barabarani.
Mara baada ya kukabidhiwa cheti cha heshima kwa mchango, Airtel Tanzania wamesema wataendelea na kampeni yao ya kuhakikisha ujumbe wa usalama barabarani “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA” unafikia walengwa wote kupitia njia mbalimbali za mawasiliano “Airtel Tanzania tunaendelea na dhamira yetu ya kuhakikisha Usalama Barabarani pamoja na kupunguza vifo vya ndugu zetu kutokana na ajali vinapungua, hivyo tumeanza kutuma ujumbe mfupi (SMS) kwa wateja wetu nchini kuwasihi kuheshimu sheria barabarani ili kuokoa maisha ya wengine alisema Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando.
Airtel Tanzania ni wadhamini wa kampeni hii ya nenda kwa usalama barabarani kwa miaka mitano mfululizo sasa na kwa mwaka huu Airtel imejitolea uchapishaji wa stika za usalama barabarani pamoja na hilo pia Airtel imeshaweka mabango yenye kutoa tahadhari za barabarani kwa abiria na madereva katika barabara mbalimbali zilizopo nchini kwa lengo la kupunguza ajali zinazotokea mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...