SHINDANO la ‘Bibi Bomba’ ambalo lilikuwa likiratibiwa na kituo cha Clouds TV, usiku wa kuamkia leo limefikia tamati na Veronica Mpangala akiibuka mshindi wa kitita cha 5,000, 000/= (milioni tano) huku nafasi ya pili ikitwaliwa na Anna Saidi ambaye alijipatia kiasi cha shilingi milioni tatu, na ukurasa wa washindi ukifungwa na Nasra Mohamed ambaye alijitwalia kiasi cha shilingi milioni moja na nusu.
Washiriki wengine watano ambao walikuwa wamesalia kwenye shindano hilo walipatiwa zawadi kila mmoja na watu mbalimbali waliokuwa wamealikwa kwa ajili ya kufanikisha zoezi hilo.


No comments:
Post a Comment