Friday, August 3, 2012

STARS KUIKABILI BOTSWANA AGOSTI 15



Said Bahanuzi 'Spider Man', mshambuliaji mpya Stars



TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Agosti 15 mwaka huu itapambana na Botswana ‘Zebras’ katika mchezo maalumu wa Kalenda ya FIFA utakaofanyika jijini Gaborone.
Tayari Kocha Kim Poulsen alishatangaza kikosi cha wachezaji 21 kitakachoingia kambini Agosti 8 mwaka huu tayari kwa mechi hiyo ya kirafiki ya kujipima nguvu.
Wachezaji wote walioitwa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager wanatakiwa kuripoti kambi kwenye hoteli ya Tansoma, Dar es Salaam, Agosti 8 mwaka huu saa 1 jioni tayari kwa mazoezi yatakayoanza siku inayofuata.
Makipa walioitwa kwenye kikosi hicho ni Deogratias Munishi (Azam), nahodha Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni nahodha msaidizi Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba).
Viungo ni Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Moshi (Simba), Mrisho Ngassa (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Ramadhan Chombo (Azam), Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar). Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samatta (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Said Bahanuzi (Yanga), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC).

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...