Tuesday, August 21, 2012

SHEREHE ZA IDD; MANENO OSWALD AMDUNDA RASHID MATUMLA, NATURE, MAUNDA, MWASITI, LINAH, JAHAZI WAFUNIKA.


Bondia Maneno Oswald akitangazwa baada ya kumdunda Rashid Matumla.

MPAMBANO wa ndondi baina ya mabondia Maneno Oswald na Rashid Matumla ambao ulifanyika ukumbi wa maraha wa Dar Live Mbagala, jijini Dar es Salaam, katika kuadhimisha sikukuu ya Idd el Fitr, ulishuhudia Oswald akimchakaza Matumla kwa pointi.
Mbali na mpambano huo uliofanyika usiku wa kuamkia jana, kulikuwa pia na burudani za aina mbalimbali, likiwemo disko la watoto ambao pia walifurahia kuogelea katika bwawa maalum na michezo mingine mingi. Kwa upande wa muziki kulikuwa na shoo kali zilizofanywa na wanamuziki Juma Nature, Mwasiti Almasi, Estelinah Sanga ‘Linah’, Maunda Zorro na kundi zima la Jahazi Modern Taarab likiongozwa na mfalme, Mzee Yusuf.
Matumla akisulubiwa jukwaani wakati wa mpambano huo.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Juma Kassim ‘Juma Nature’, akionyesha ukongwe wake.
Kiongozi wa Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf akiwapagawisha mashabiki zake.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Estelinah Sanga ‘Linah’, akiwa jukwaani.
Mwasiti Almasi akikamua na wacheza shoo wake.
Maunda Zorro akionyesha umaarufu wake.
Sadick Momba (kushoto), akipambana na Venance Mponji katika mpambano wa utangulizi ambapo Sadick aliibuka mshindi.
Julius Thomas (kushoto), akizidunda na Jumanne Kirumbe kabla ya Maneno Oswald na Matumla kupanda ulingoni. Julius alishinda mpambano huo.
Mmoja wa wasanii wa kundi la Mabaga Fresh ambaye sasa yuko katika kundi la Wanaume Halisi, JB Mkuu wa Maadui akiwajibika.
Mwimbaji wa Bendi ya Jahazi Modern Taarab, Khadija Yusuf akitumbiza jukwaani.
Malkia wa Bendi ya Jahazi Modern Taarab, Leila Rashid akiwajibika.
Watoto wakicheza muziki ndani ya bwawa la kuogelea.
Baadhi ya umati uliokuwa ndani ya ukumbi huo.



No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...