Friday, August 10, 2012

MASHUJAA MUSICA KURUDI MIKOANI KWA KISHINDO


Baadhi ya wasanii wa Bendi ya Mashujaa wakiwa katika pozi la pamoja.

BENDI ya muziki wa dansi Mashujaa Wana kibega wiki hii walifanya ziara ya maalum katika mikoa ya Mbeya na Ruvuma kwa ajili ya kutambulisha wanamuzi wao wapya pamoja na nyimbo yao ya RISASI KIDOLE utunzi wake Charles Gabriel Mbwana almaalufu Chazbaba Toress.


Akizungumza jana Meneja wa bendi hiyo Martin
Sospeter, alisema kuwa wanamuziki wa bendi hiyo waliondoka siku ya  Alhamis kuelekea Mkoani Ruvuma na kufanya onyesho lililofana na kukonga nyoyo za mashabiki wa mji wa Songea katika mwezi huu wa Ramadhani. Meneja Sospeter alisema onyesho la kwanza lilitafanyika kwenye Ukumbi wa Serengeti Club uliopo mjini Songea siku ya Ijumaa na baadaye siku ya Jumamosi kwenye ukumbi wa Live uliopo Mbeya Mjini na siku ya Jumapili walimalizia onyesho lao kwa bonanza maalum lililofanyika kwenye ukumbi wa Mbeya City Pub Mbeya mjini.
Meneja Martin Sospeter aliongeza kuwa katika ziara hiyo ambayo lengo lake lilikuwa ni kutambulisha safu mpya ya bendi hiyo na mtindo wao mpya wa Kibega mambo yalikwenda kama walivyokusudia. Bendi hiyo imerejea Dar es Salaam jana Jumatano na
itaendelea na ratiba zake kama kawaida katika kwa ajili ya kuwakonga mashabiki wao kwenye kumbi tofauti za jijini Dar es Salaam kadri watakavyoona inafaa.
Kumbukumbu zinaonyesha kuwa bendi hii hivi karibuni ilifanya mabadiliko makubwa kwa kuchukuwa wanamuziki wapya ambao ni Charles Gabriel 'Chalz Baba', Soud Mohamed MCD' na Lilian Tungaraza Lilian Internet wote kutoka The African Stars Twanga Pepeta.
Wengine ni Saulo John kutoka katika bendi ya Extra Bongo na Ali Akida mwanamuziki huru. Pamoja na Meneja Martin kutoka Twanga Pepeta ambao wote kwa pamoja wamedai kuwa wameenda kwasababu ya Maslahi. Swali linakuja je maslahi yatakapofikia ukingoni nini kitafuata????

Hawa ndiyo waliyowahi kuhama Bendi ya Twanga Pepeta na kwenda kupiga mzigo kwenye bendi tofauti tofauti kwa madai ya kujiongezea kipato, wakiwa na mmoja wao wa (kwanza kutoka kulia), Jose Mara ambaye yeye alihama bendi akitokea bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma,.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...