Mdau wa Sanaa na mkongwe wa muziki wa dansi nchini John Kitime (kushoto) akisistiza jambo wakati akiwasilisha mada kuhusu Historia ya Muziki nchini kwenye Jukwaa la Sanaa wiki hii. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idaya ya Ukuzaji Sanaa BASATA Vivian Shalua na Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari Godfrey Mungereza.
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limevitaka vyombo vya habari kuwa mstari wa
mbele katika kudhibiti kazi za Sanaa zisizo na maadili kabla ya kwenda
hewani ili kuepuka mmomonyoko wa maadili katika jamii.
Wito
huo umetolewa mapema wiki hii na Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Sanaa
BASATA Vivian Shalua wakati akiiahirisha programu ya Jukwaa la Sanaa
inayofanyika kila wiki kwenye Ukumbi wa BASATA ulioko Ilala Sharif
Shamba jijini Dar es Salaam.
Alisema
kuwa, wakati Baraza limefikia hatua nzuri ya kudhibiti hali hiyo, wadau
wakuu katika kumaliza tatizo hili ni wasanii wanaotakiwa kutunga kazi
bora na zenye maadili huku vyombo vya habari vikiwa na wajibu wa kuchuja
kila kazi ya Sanaa inayopokelewa kabla ya kuirusha hewani.
“Basata
imeshaviandikia vyombo vya habari kuvielekeza kuwa na kamati za ndani
za kudhibiti maadili kwenye kazi za sanaa kabla ya hazijaenda hewani.
Hili ni muhimu sana katika kujenga maadili ya mtanzania” alisisitiza
Shalua.
Awali akiwasilisha mada kuhusu Historia ya Muziki nchini na hatua zake
mkongwe wa muziki wa dansi nchini John Kitime alisema kuwa, kumekuwa na
changamoto mbalimbali miongoni mwa wasanii wa fani hiyo hali
inayoufanya usifike mbali.
Alizitaja
baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na wasanii kutozingatia sheria
ya hakimiliki na hakishiriki iliyopo, kuiga midundo ya muziki kutoka
nje hali inayosababisha kutokuwepo kwa muziki wenye utambulisho wa
Tanzania kama ilivyo kwa mataifa mengine ya Afrika hususan Afrika
Kusini.
“Tatizo
kubwa ni wasanii wetu kuiga miziki na hata tamaduni za kigeni, hatuwezi
kuandaa kazi za Sanaa kufurahisha wazungu au watu kutoka nje tu,
tutapotea” alionya Kitime.
Kwa
upande wake Rais wa Shindano la ulimbwende la Utalii (Miss Utalii)
Gideon Chipungahelo alisema kuwa, kihistoria wanamuziki wetu ukianza na
wakongwe waliopo walijikita katika kuiga miziki ya Zaire hivyo
kinachofanywa na wasanii wetu wa sasa ni mwendelezo tu.
“Ni
wazi kazi iliyopo sasa ni kuwafanya wasanii kujikita katika utajiri
mwingi wa makabila yenye midundo mbalimbali tuliojaaliwa. Hapa ndipo
tunapaswa kusisitiza” alishauri Chipungajelo.
No comments:
Post a Comment