Wednesday, July 25, 2012

YANGA, AZAM, VITA SC NA APR KUVAANA NUSU FAINALI KESHO TAIFA



Kikosi cha Timu ya Yanga SC kikiwa katika picha ya pamoja tayari kwa mchezo wa nusu Fainali ya Kombe la Kagame zidi ya timu ya APR ya Burudi ambayo itachezwa saa 10 jioni.

Wachezaji wa Timu ya Azam wakishangilia muda mfupi baada ya kuichapa goli tatu timu ya wekundu wa Msimbazi katika mchezo wa robo fainali iliyofanyika jana jioni uwanja wa Taifa.

MICHEZO ya nusu fainali ya kuwania kombe la  Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Kombe la Kagame 2012, zinatarajiwa kuchezwa kesho katika  Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Azam na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) zitacheza nusu fainali ya kwanza kuanzia saa 8 kamili mchana, na kufuatiwa na nusu fainali ya pili kati ya Yanga na APR ya Rwanda itakayoanza saa 10 kamili jioni.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...