Sunday, July 22, 2012

RAIS DK SHEIN AWAONGOZA VIONGOZI NA WANANCHI KATIKA DUA YA HITMA KUWAOMBEA WALIOKUFA KWA AJALI YA MELI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein, leo ameungana na viongozi mbali mbali wa Kitaifa katika dua
maalum ya hitma pamoja na Sala maalum ya Maiti (Salatul Mayyit
al-ghaib), iliyosomwa huko katika msikiti Mushawar, Mwembeshauri mjini
Zanzibar.

Sala na dua hiyo ni maalum kwa ajili ya kuwaombea watu waliokufa
kutokana na ajali ya kuzama kwa meli ya MV SKAGIT, iliyotokea hivi
karibuni wakati meli hiyo ilipokuwa inasafiri kutoka Dar-es-Salaam
kuja Zanzibar na kusababisha vifo na majeruhi kadhaa

Katika sala na dua hiyo viongozi mbali mbali wa dini, vyama na
Serikali walihudhuria akiwemo Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muunganao
wa Tanzania Mhe. Dk. Mohammed Kharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idd, Rais mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dk.
Amani Abeid Karume.

Viongozi wengine waliohudhuria ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar
Khabh, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Spika wa Baraza la
Wawakishi Mhe. Pandu Ameir Kificho, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib
Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis, Mawaziri, Manaibu Waziri, Wabunge,
Wawakilishi, Mashekhe mbali mbali wa Zanzibar na Tanzania Bara pamoja
na wananchi na viongozi wengine.

Hitma ya Waliokufa kwa Ajali ya Meli hivi karibuni

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein,(wa tano kushoto) pamja na
Viongozi wengine wa Serikali wakiungana na Waislamu katika Swala ya
kuwaombea Dua Abiria waliofariki katika Ajali ya Meli Mv Skagit ya
Kampuni ya Seagul,iliyozama hivikaribuni ikitokea Dar es Salaam
kuelekea Zanzibar,swala hiyo ikiongozwa na Mufti wa Zanzibar Sheikh
Saleh Omar Kabi,katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein,(katikati) pamja na Viongozi wengine wa
Serikali wakiungana na Waislamu katika Hitma ya kuwaombea Dua
Abiria waliofariki katika Ajali ya Meli Mv Skagit ya Kampuni ya
Seagul,iliyozama hivikaribuni ikitokea Dar es Salaam kuelekea
Zanzibar, katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar leo.[Picha na
Ramadhan Othman Ikulu.]

Baadhi ya Waislamu waliohudhuria katika Hitma ya
kuwaombea Dua Abiria waliofariki katika Ajali ya Meli Mv Skagit ya
Kampuni ya Seagul,iliyozama hivikaribuni ikitokea Dar es Salaam
kuelekea Zanzibar, katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...