Saturday, July 14, 2012



KOCHA Mkuu wa Simba Milovan Cirkovic amesema kikosi chake hakipo imara katika kiwango kile anachokihitaji kwa ajili ya Michuano ya Kagame ambayo timu nyingi zinajiandaa vizuri.
Wachezaji ambao viwango vyao havijamridhisha ni Haruna Moshi ‘Bobani’, Mwinyi Kazimoto, Juma Nyosso na Amir Maftar na hivyo amepanga kuwapa mazoezi kuwarudisha kwenye line.
Simba inatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza Jumatatu ijayo na URA ya Uganda saa kumi jioni na mchezo mwingine utapigwa kati ya Villa Club na Ports saa 8:00 mchana kwenye Uwanja wa Taifa.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...