Wednesday, July 25, 2012

BENDI YA EXTRA BONGO YAZINDUA ALBAM MPYA ULAYA




BENDI ya Extra Bongo iliyo chini ya Mkurugenzi wake Ally Chocky, imezindua Albam yao ya 'Mtenda akitendawa hujihisi kaonewa' barani Ulaya wakiwa katika ziara yao nchini Finland.

Akizungumza kwa njia ya mtandao Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Chocky, amesema kuwa wameamua kuzindua albam yao hiyo yenye jumla ya nyimbo saba, nchini Finland baada ya ashabiki wao wa nchini humo kuwataka kufanya hivyo ili waweze kuzipata nyimbo zote za bendi hiyo.

Aidha Chocky amesema kuwa baada ya kupokea ombi hilo kutoka kwa mashabiki wao hakuweza kupinga kutokana na hamasa iliyojitokeza wakati wa mapokezi yao nchini humo na wakati wa maonyesho yao katika Tamasha la First Afrika.

Choky alisema kuwa baada ya uzinduzi huo sasa mbali na kuwa bendi hiyo bado iko nje ya nchi lakini albam yao sasa inapatikana katika maduka yote na kuuza kanda jijini Dar es Salaam na mikoani kwa ujumla.

Alizitaja nyibo zilizomo kwenye albam hiyo kuwa ni pamoja na Mtenda akitendewa, uliotungwa na yeye mwenyewe Ally Chocky, Falsafa ya Maisha utunzi wake Banza Stone, Ufisadi wa Mapenzi utunzi wa Robert Hega, Mashuu wa Ally Chocky, Neema utunzi wa Athanas Motanabe, Bakutuka uliotungafu ya wanenguaji wa bendi hiyo, Super Nyamwela na Extra Bongo Shoo.

EXTRA BONGO BAND ALBUM
Artists: ALI CHOCKY & EXTRA BONGO BAND
ALBUM: MTENDA AKITENDWA

TRACK LIST:
1. MTENDA - ALI CHOCKY
2. FALSAFA YA MAISHA - BANZA STONE
3. UFISADI WA MAPENZI - ROBERT HEGGA CATERPILLAR
4. MASHUU - ALI CHOCKY
5. NEEMA - ATHANAS
6. BATUKUTA - SUPER NYAMWELA
7. EXTRA BONGO SHOW - BONUS TRACK

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...