Wednesday, July 18, 2012

AJALI YA MELI YA SEAGULL YASABABISHA BUNGE KUSITISHWA


Meli ya SKAGET ambayo ni mali ya kampuni ya SEAGULL, ikizama baharini huko Chumbe visiwani Zanzibar muda mfupi baada ya kuondoka bandarini jijini Dar es Salam ikiwa na abiria wanaokadiriwa kufikia 250 waliokuwa wakisafiri kwenda mjini Zanzibar.
 
Hii ndiyo meli iliyozama huko Chumbe Zanzibar. Hapa ikiwa katika bandari ya Dar es Salaam ikipakia abiria

Spika wa Bunge, Anne Makinda leo jioni amesitisha shughuli za bunge kufuatia ajali ya meli ya Mv Seagull, iliyozama leo katika Bahari ya Hindi ikitokea Dar es Salaam kwenda Pemba,'. Abiria wapatao 250 wanahofia kufa. Lakini habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba watu 12 wameopolewa wakiwa wamekufa.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...