Monday, June 11, 2012


KOCHA Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall anatarajiwa kuwasili nchini leo asubuhi kwa ajili ya kuanza program ya maandalizi kwa mashindano ya kombe la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Stewart alikuwa nchini Uingereza kwa mapumziko baada ya kumaliza msimu uliopita kwa mafanikio ya kutwaa medali ya fedha kwa kuwa washindi wa pili wa VPL.
Katibu Mkuu wa Azam FC, Nassor Idrissa jana ameiambia tovuti ya http://www.azamfc.co.tz/ kuwa wataanza mazoezi jioni kutokana na kocha huyo kurudi asubuhi ya siku hiyo.
Akizungumzia wachezaji wengine alisema, wachezaji wote wa kimataifa wameshawasili tayari kwa kuanza mazoezi hayo wakiwa pamoja na wachezaji wengine. Mazoezi hayo yatafanyika kwenye uwanja wa Azam Chamazi jijini Dar es Salaam.
Idrissa aliongeza kuwa wachezaji waliopo timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ watajiunga mara baada yakumaliza michezo yao, na wale wa Zanzibar Heroes watarejea nchini baada ya kumaliza michezo ya Kombe laDunia kwa nchini ambazo sio wanachama wa FIFA.
Aliwataja wachezaji waliowasili kuwa ni George Odhiambo na Ibrahim Shikanda kutoka nchini Kenya ambao wotewaliingia Alhamis, Tchetche Kipre na Michael Kipre kutoka nchini Ivory na Joseph Owino wa Uganda.
Idrissa alisema wachezaji wa Tanzania nao wameshaandaa mazingira kwa ajili ya kuanza mazoezi hayowakiwemo vijana kutoka Azam Academy ambao wamepanda kuicheza timu kubwa, Aishi Salum, JucksonWandwi, Dizana Issa, Ibrahim Rajab ‘Jeba’ na Joseph Kimwaga.
Aidha Idrissa alisema Azam Academy wameshaanza mazoezi siku ya Ijumaa isipokuwa wacheza watatu ambaobado hawajawasili kujiunga na timu hiyo

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...