Monday, June 18, 2012

MILLARD AYO AFUNGUKA KWA MO BLOG JUU YA AJALI MBAYA ILIYOWAHI KUMTOKEA MAISHANI.

PIA AZUNGUMZIA JINSI ALIVYOONDOKA RADIO ONE NA UHUSIANO WAKE NA MKURUGENZI WA ITV/RADIO ONE.

SEHEMU YA KWANZA.
Kama ilivyo kawaida kwa wataalamu wa masuala ya habari na kijamii , Mhariri Mkuu wa Mtandao huo Lemmy Hipolite na Meneja Mipango Zainul Mzige ‘hamad’ uso kwa uso na mtangazaji maarufu wa Radio na Televisheni hapa nchini Millard Ayo.
LEMMY: Haya ndugu yangu za masiku hatuonani ila mimi nakuona tu kwenye luninga.
AYO: Aiyaa….! Wakuu ni aje ni kitambo kimepita hatujaonana ila mimi niko poa tu nakaza buti.
ZAINUL: Usiende mbali tunajua uko bize lakini hebu kaa kitako uzungumze na mhariri wangu kuhusu mawili matatu watu wasio yajua kuhusu wewe.
MO BLOG: Nini kimeshawahi kukutokea maishani ambacho huwezi kukisahau na wasikilizaji na watazamaji wako hawakifahamu.
MILLARD AYO: Nilishawahi kupata ajali mbaya kiasi kwamba watu wengi wasingekuwa wananifahamu hivi leo. Ni ajali ambayo iliondoka na rafiki zangu wanne.
MO BLOG: Pole sana na tuna muomba Mwenyezi Mungu Mwenye Rehema Awarehemu.
MILLARD AYO: Amina.

Tulikuwa tunasafiri na basi katika safari za kishule, tulikuwa 60 hivi kwenye basi tukapata ajali ‘Ngongoro crater’ bonde la ufa sehemu inaitwa ‘Malanjo Cross’ ni sehemu hatari sana, yaani tuliingia bondeni, yaani sidhani kama leo ningekuwa hai.



MO BLOG: Hebu Millard tufafanulie zaidi tukio hilo la ajali lilikuaje..?

MILLARD AYO: Yaani sina la kusema ila kama Mungu asingependa mimi nisingekuwepo duniani, lakini kwa sababu alipenda, ndio maana nipo, hata hili kovu katika kichwa upande wa kushoto lipo. Hapa iliingia chuma, unajua mabasi ya zamani yalikuwa na chuma, sasa ile chuma ilikatika wakati basi likijipiga kwenye mawe kama unavyojua kule ni crater.
Kwa kweli ninachokumbuka ni kuwa gari lilipotulia watu walikuwa wakilia na damu zinatiririka na mimi nilikuwa nimebanwa katika hiyo chuma na nilipotolewa sikukumbuka tena nini kiliendelea.
Ilikuwa mbaya sana kwa sababu lile basi lilikuwa likibiringika kama chupa, hivyo watu wanatupwa madirishani na kisha gari linawalalia ndio mazingira watu walivyopoteza maisha.

OMG…!!!



MO BLOG: Kitu kingine ambacho MO BLOG ingependa kufahamu ni kuondoka kwako ITV, fununu zinasema kuwa ulikuwa ni mtiti, ni ya kweli haya?


MILLARD AYO: Ningependa watu wakifahamu ni kuwa mimi sina ugomvi na ITV wala sikuondoka kwa ugomvi.
Kwanza kufanya kwangu kazi ITV naamini Mungu alikuwa anaona na alipanga ndio maana hata hivi sasa kuna uwezekano kuwa nafasi nyingine nilizo nazo maishani kwangu nisingezipata, pengine hata ‘Clouds’ wasingeniona na wasingenifuata.
ITV ndio ilimtambulisha Millard Ayo.
ITV niliondoka vizuri ndio maana nitawaheshimu na nitazidi kuwatangaza vizuri popote nitakapokwenda.
Kwa sasa hapa ‘Clouds Radio’ nafanya show yangu ya ‘Amplifaya’ ambayo ina sehemu inayohusisha Blogs, Facebook na Twitter.
Katika kipengele hicho nasoma sana habari zao wanazo zi’tweet’ na nasema nimezitoa ITV.



MO BLOG: Zungumzia mahusiano yako na viongozi wa ITV na wafanyakazi wake.

MILLARD AYO: Nasema ukweli kuwa sina kinyongo na Mkurugenzi Mkuu wa ITV Joyce Mhaville tena namwambia asante sana kwa kunilea, sina matatizo na waliokuwa wafanyakazi wenzangi wa ITV na Radio One na tunaendelea kuwasiliana kama kawaida na nawaambia tuko pamoja na nawapenda sana.

Wengine tunakutana na tunakuwa ‘good times’ pamoja na bado nitaendelea kuwaheshimu kote nilikotoka ikiwemo ITV, WAPO RADIO na TVZ, hata kama kuna mapungufu, hakuna sehemu isiyokuwa na mapungufu.

Wasikilizaji wa ‘Amplifaya’ msisite kusikiza kipindi hiki kwa sababu kila unachokipenda utakipata humu

Msomaji wa Blog hii usikose SEHEMU YA PILI ya mahijiano ya MO BLOG na MILLARD AYO ambapo amezungumzia maisha yake ya kimapenzi na suala tata linalovuma hivi sasa la ‘FREEMASON’.



Millard Ayo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mhariri Mkuu wa MO BLOG Lemmy Hipolite (kushoto) na Assistant Operation Manager wa MO BLOG (kulia).



Millard Ayo (katikati) akishow love na Mhariri Mkuu wa MO BLOG Lemmy Hipolite na Mpiga picha wa MO BLOG Geofrey Mwakibete (kulia).
Habari/picha:MO BLOG

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...