MCHUNGAJI GETRUDE RWAKATARE AWAMBIA WAUMINI WAKE KUWA SOMO LA JUMAPILI NI LAKUKUNJA USO, TOFAUTI NA MASOMO YALIYOPITA
Mchungaji Getrude Rwakatare
Waumini
Mchungaji
wa Mlima wa Oto Mikocheni B aliwaambia waumini wake kuwa leo wanalishwa
ndimu na sio chakula kitamu maana somo la leo litagusa maisha yako kwa
kiwango kikubwa. Na somo lilikuwa kama ifutatavyo:
Mchungaji Rwakatare: Bwana Yesu asifiweeeeeee
Waumini: Ameeeeeni
Mchungaji Rwakatare: Leo nimekuja na uso wa ndimu, nawalisha chakula ambacho hamjawahi kula. Leo tutajifunza
MAOMBI YA VITA
Ufunuo
12:7, Petro 5:8-9)
-Shetani
alifukuzwa mbinguni na kutupwa duniani kutokana na uovu wake. Shetani amekuwa
kikwazo kikubwa sana kwa wanadamu kwa kuanzisha
vita vya kiroho, na Mungu anasema vita vyetu kama
wanadamu si vya kimwili bali ni vya kiroho dhidi ya adui shetani. Hatuwezi
kupambana naye kimwili kwasababu hatumuoni.
Waimbaji wa Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B, Joy Bringers
Maombi ndio silaha na ni dawa kwa kila amwaminiye BWANA. Kwa kupitia maombi yako kwa Mungu unaweza pia kupambana na shetani. Watu wengi wakati wa maombi wanadharau, utaona wengine wanakosa hata heshima katika kipindi cha maombi, watu wanatafuna bigijii, wanaongeaongea, wanaachama midomo
Wachungaji
wetu wanapaswa kukumbushwa wakati wa maombi. Kuna baadhi ya wachungaji
hawasisitizii waumini wao kuomba na badala yake wanaweka fedha mbele na kusahau
kuwa hizo pesa zinakuja kwa msaada wa maombi.
Watu
wamechukulia maombi kama ni kitu cha kawaida, na shetani anapoona huombi
anafurahi sana na ni rahisi sana kwake kukuingia kwasababu kunakuwa
hakuna kipingamizi chochote ndani yako (huna silaha yoyote ya kumzuia shetani)
Waumini
(Mathayo 11:12)
Waumini
(Mathayo 11:12)
Ufalme wa
Mungu hukuongezea matumaini. Watu wengi wanafurahia sana
kuona maombezi ya Nabii TB Joshua wa Nigeria akiombea watu mbalimbali,
lakini cha kujiuliza ni kwamba, unafaidika nini unapoona wengine wanaombewa na
wewe umekuwa ni mtazamaji tu? Wengine wanapona na wewe umebaki na ugonjwa wako,
wengine wanapata safari za Ulaya wewe bado ukouko tu. Simama kama wewe, omba
kwa Mungu wako kwa juhudi zako zote, Na kumbuka huwezi kupokea kwa Mungu kama
hujatubu dhambi zako kwanza kabla ya maombi nakusamehe waliokukosea. Mungu
huangalia mioyo iliyosafi na sio iliyochafuliwa na maovu.
Huwezi
kumshinda sheatani kwa kuimba mapambio tu bila ya kuwa na Mungu ndani yako kwa
kupitia Roho Mtakatifu. Pia ka,a ,ao,bi yako ni kilelemama huwezi kufanikiwa,
maombi yako yawe na nguvu mbele za Mungu. Hii ninamaanisha ombi kwa kumaanisha
na kuwa na imani unahoomba kinatendeka. Ukiwa huna imani na kile unaomba
hutafanikiwa na hutapokea chochote.
KWANINI NI
LAZIMA KUPAMBANA NA SHETANI?
1/ Kujitetea mwenyewe
-Sheatni
hutakutafuta huku na huku ili akumeze (Yakobo 4:7, Yohana 10:16). Shetani huja
ili aibe na aharibu kile ulichonacho. Shetani anaweza kumtumia rafiki au ndugu
ayko kukuharibia mipango yako, kwahiyo hupaswi kumchukia ndugu yako au rafiki
yako aliyekukwaza ila mchukie shatani.
Tenga Muda
wa maombi na sehemu ya kufanyia maombi, kama
ni chumbani, funga milango yako na aanza maombi.
Usikubali
kudharaulika, kuonewa, kusemwa, kusengenywa, kwa wewe ni motto wa Mungu
2/ Kurejesha kile kilichochukuliwa na shetani
Kama wewe
umeibiwa mchumba wako, mume wako, mali zako au unakesi ya
kusingiziwa, ukiwa na Mungu na ukamwani na kumtumikia vyema, hivyo vyote
vitarudishwa.
Amgali sana watu unaowakopesha
wengine huwa hawarudishi pesa baada ya kukopa. Kama
utakutana na mwamini wa Mlima wa Moto Mikocheni B amnataka kukukopa pesa zaidi
ya 50,000 naomba unitaarifu mchungaji wako na mimi nitakula naye sahani moja.
Mara nyingi
shetani anapokuwa ameingia kwako, hapendi kutoka, ni lazima ufanye kazi ya
ziada kumuondoa ili baraka zako zirudi. Shetani huzuia barajka zako au
mafanikio yako anapokuwa ndani yako
Wachawi
lazima wauawe kwani si wazuri katika maisha yako, na mchawi utamuua kwa maombi
na sio kwa kutumia silaha za kimwili. Kuna watu wangekuwa mbali katika maisha yao lakini shetani
amekalia baraka zao
(Methali
6:31) Mtu anayekuloga anakualibia utukufu wako.
3/
Kujifungua katika kifungu cha shetani
Tunaaswa
kufanya maombi ya kutaa kazi za shetani kwa kukata mifungo vyake vyote. Kuna
vifungo mbalimbali:-Mafanikio, maendeleo katika maisha yako n.k.
Mungu
anataka utoke mahali hapo nauende mahali pengine, na unaweza kutoka kama utakuwa umeweka maisha yako kwa Yesu na kuwa mtu
unayefanya kazi za Mungu na kuachana na dhambi. Kusoma Neno la Mungu kila
wakati ili kuidumisha imani yako.
Shetani
hana raha anapoona wewe unafanikiwa katika maisha yako, anapata taabu sana anapoona unatumia
jina la Yesu kwa kuyafanikisha maisha yako.
Usikubali
kulindwa na shetani mabaye haonekani kwa macho. Tuwe watu wa maombi sana na watakatifu.
Kumbuka maombi ya usiku yana nguvu sana
mbele za Mungu.
Ukitaka
kujiinua lazima ujitakase nikimaanisha usiwe na doa la dhambi kwa kutubu maovu
yako. Unapofanya mabaya unamruhusu shetani kuingia kwako. Dhambi ni chukizo
mbele za Mungu.
4/ Ni haki
mbele za Mungu kuwalipa wale watutesao, misukosuko na mihangaiko.
(Wathesalonike
2:1)
Ni haki
kulipa misukosuko kwa watu wateswao na misukosuko na kuwapa raha. Si haki kwao
kuwa na maisha ya kubahatisha.
Watu
wanakosa maarifa ya kuwangusha shetani, kwa kutumia jina la Yesu ambalo ni
ngome a,bapo watu wenye haki hulikimbilia na kuwa imara
(Wakoritho
2:10:3-6, Methali 18:10, Ufunuo 12:11)
Silaha za
Mungu ambazo unaweza kuzitumia ni kama :-
a/ Moto wa
Mungu
b/ Damu ya
Yesu
c/ Sifa
(Nyakati
2:20)
No comments:
Post a Comment