Thursday, June 7, 2012

MANJI 'AJILIPUA' YANGA, VIGOGO SERIKALINI WAINGIA MITINI


Manji; Mwenyekiti mpya mtarajiwa Yanga

YUSSUF Mehboob Manji ni miongoni mwa wanachama 29 wa Yanga waliorudisha fomu  kwa ajili ya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika klabu hiyo, katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Julai 15, mwaka huu, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Francis Kaswahili alisema hayo katika Mkutano na Waandishi wa Habari kwamba, Manji ni miongoni mwa wanachama wanne waliorudisha fomu kwa nafasi ya Mwenyekiti, wengine wakiwa ni John Jambele, Edgar Chibura na Sarah Ramadhani.
Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Kaswahili aliyekuwa akizungumza mbele ya mwakilishi wa kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Hassan Chabanga Dyamwale alisema wamerudisha wanachama watano ambao ni Ally Mayay, Ayoub Nyenzi, Yono Kevela na Clement Sanga.
Katika nafasi za Ujumbe waliorudisha ni Lameck Nyambaya, Ramadhani Mzimba ‘Kampira’, Mohamed Mbaraka, Ramadhani Said, Edgar Fongo, Beda Simba, Ahmad Gao, Mussa Katabaro, George Manyama, Aaron Nyanda, Abdallah Bin Kleb, Omary Ndula, Shaaban Katwila, Jumanne Mohamed Mwammenywa, Abdallah Mbaraka, Peter Haule, Justin Baruti na Abdallah Sharia.
Kaswahili alisema Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, Mfanyabiashara Muzamil Katunzi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Eliakhim Masu hawakurudisha fomu, wakati Isaac Chanzi pia hakurudisha fomu ya Makamu Mwenyekiti.


Mzee Dyamwale kulia akifafanua jambo kwa Waandishi kumsaidia Kaswahili.
 
PICHA/HABARI: BINZUBEIR BLOG

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...