JOHN SHABANI AGUSA MIOYO YA WATANZANIA
John shabani akimsindikiza Mheshimiwa Fenella Mukangara
(Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na michchezo)
Tarehe 10.06.2012, ilibaki kuwa siku ya historia kwa
maelfu ya watu katika jiji la Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla. Ni lile tamasha la kusifu na kuabudu pamoja na maombi
maalum kwa ajili ya nchi ya Tanzania, ambalo liliandaliwa na mtumishi wa Mungu
John Shabani .
Katika tamasha hili mgeni rasmi alikua Waziri wa habari vijana utamaduni na michezo,
Mh Dr Fenella Mukangara.Mh Mukangara baada
ya kuzindua DVD na BLOG ya John Shabani, pia ameongoza harambee ya kuchangia
huduma ya mtumishi huyo wa Mungu
Mamia Ya Wakazi wa Jiji la Dar-es-Salaam
walijitokeza kwa Wingi Katika Tamasha hilo ili Ku-m-Support Mwanamuziki
Nguli wa Muziki wa Injili John Shabani lililofanyika Katika Kanisa la TAG
Magomeni.
Moja kati ya matukio muhimu katika
tamasha hili linaloendelea hapa ni uwepo wa wakongwe wa injili nchini Mzee
makasi, Mzee Cosmas Chidumule.Pamoja na hayo Upendo Kilahilo pamoja na Stara Thomas
aliye okoka hivi karibuni. John Shabani,
Upendo Kilahiro pamoja na Apostle John Komanya walipanda jukwaani na kuimba kwa
pamoja wimbo wa tenzi uitwao KALE NILITEMBEA amabao kimsingi umegusa
mioyo ya wengi. Wimbo huo ni miongoni mwa nyimbo kali zilizomo katika albam
mpya ya John Shabani, Album hiyo inasimamiwa na Kampuni ya Msama Promotion na
inategemea kuwa tayari muda si mrefu. Nyimbo zingine zilizomo katika album hiyo
ni pamoja na
Kwa
Yesu kuna raha – John Ft Cosmas
Chidumule
Tunaye
Baba – John Ft Jane Misso
Wewe
ni Baba – John Ft Faraja Ntaboba
(DRC Kongo)
Mungu
yu mwema – John ft. Christina Matai
Nimemwona
Bwana – John ft. Tina Marego
Akisema
Ndio – John ft. Destiny Sisters
(Kampala)
Wakati
wangu – John ft. Bella Kombo
Katika tamasha hili rangi iliyotawala
ni Red kama ionekanavyo pichani na pia limehudhuriwa na Rais wa waimbaji nchini
Mtumishi Addo November. Waimbaji
wengi pamoja na kwaya na vikundi mbalimbali wamehudhuria katika tamasha hilo.
Pia waandishi mbalimbali wa habari na vyombo mbalimbali vya habari vikiongoza
na Television ya taifa TBC vilikuwepo. Maombi maalumu kwa ajili ya Nchi yetu
yameongozwa Na Mchungaji Danstan Kanemba pamoja na Bishop Rechael.
John Akiimba kwa hisia
John Shabani akishusha uwepo jukwaani
John Shabani akiagana na Mheshimiwa Waziri wa habari vijana utamaduni na michezo
Cosmas Chidumule akimsifu Mungu
Cosmas Chidumule na Stara Thomas
Mzee Makasy, mkongwe wa muziki Afrika
Victor Ahron na Rais wa Shirikisho la muziki Tanzania, mr. addo November
Martin Malechela, Addo November pamoja na Uncle Jimy
Upendo Kilahiro akiwajibika jukwaani
John Shabani na kundi lake wakifanya mambo
Watu weweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!
Upendo Kilahiro na wadau wa gospel music wakicheza kwa furaha. Mambo ya zindongazeziwelale hayooooo.
No comments:
Post a Comment