AFARIKI DUNIA BAADA YA KUDONDOKEWA NA MBAO KWENYE GARI, WAWILI WAKAMATWA NA BANGI NA 14 WAKAMATWA NA POMBE HARAMU AINA YA GONGO.
Habari na Ezekiel Kamanga,Chunya.
Mkazi wa Kijiji cha Lualanje,Wilaya
ya Chunya,Mkoani Mbeya Sani Mgavi(28),ambaye ni mwenyeji wa Wilaya ya
Mufindi Mkoani Iringa,amefariki dunia baada ya kudondokewa na mbao
wakati akijaribu kuruka kwenye gari.
Tukio hilo la marehemu ambaye ni
Fundi wa kupasua mbao,limetokea Juni 7 mwaka huu,majira ya saa 2:30
asubuhi katika kijiji hicho.
Marehemu amefariki wakati alipokuwa
akisafirisha mbao hizo na yeye akiwa nyuma ya gari aina ya Fuso lenye
nambari za usajili T 732 BWV,mali ya Bwana Joseph Paulo lililokuwa
likiendeshwa na dereva Silvesta Simkonda(48) wote ni wakazi wa wilaya
hiyo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya
Diwani Athuman,amesema chanzo cha ajali hiyo ni gari kukwama kwenye
mchanga na kuegamia upande mmoja,hali iliyompelekea marehemu kujaribu
kuruka ndipo mbao hizo zilipo mdondokea na kufariki papo hapo.
Hata hivyo mwili wa marehemu
umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Chunya na jeshi la polisi
linamshikilia dereva wa gari hilo kwa mahojiano zaidi.
Wakati huo huo Jeshi hilo
linawashikilia watu wawili kwa kosa la kukutwa na bangi gramu 15, tukio
lililotokea Juni 7 mwaka huu majira ya saa 12:55 jioni eneo la
Machinjioni,Wilaya ya Rungwe.
Kamanda Diwani amewataja waliokamatwa
kuwa ni pamoja na Damas David(31) na Lusekelo Mwakalomba,ambapo
hujihusisha na uuzaji na matumizi ya bangi hizo na wote wapo mahabusu.
Aidha majira ya saa 10:45 jioni siku
hiyo hiyo maeneo ya Katumba wilayani humo,Polisi walimkamata Bi.Sophia
Luvanda(40) pamoja na wenzake 14 wakiwa na pombe ya moshi(Gongo) lita 4
na mtambo mmoja wa kutengeneza pombe hiyo.
Watuhumiwa ni wauzaji na wanywaji wa
pombe haramu ya Gongo na mpaka sasa wote wapo mahabusu wakati upelelezi
ukiendelea kuhusiana na tukio hilo na mara baada ya upelezi kukamilika
watafikishwa mahakamani kusomewa mashitaka yanayowakabili.
No comments:
Post a Comment