MCHORO WAKUMKEJELI JACKOB ZUMA WAHARIBIWA
Watu wakitazama mchoro huo kwenye jumba la maonyesho kabla ya mchoro huo kuharibiwa. |
Mchoro unaoonyesha uume wa rais wa Afrika Kusini Jaocb Zuma ukiwa nje, umeharibiwa. Mchoro huo umezua utata nchini Afrika Kusini hasa baada ya kuwekwa katika jumba moja la maonyesho kwa umma.
Kushoto mchoro ulio haribiwa na kulia mchoro uliozua utata. |
Mtu mmoja amemwagia rangi nyeusi mchoro huo na amewaambia wandishi wa habari kuwa unamvunjia heshima rais wa nchi hiyo.
Chini ya ulinzi. |
Taarifa zinasema kuwa tayari washukiwa wawili wamekamatwa.
Waandamanaji wa ANC |
Hapo awali, chama tawala kiliitaka mahakama kuu kulazimisha wanaosimamia maonyesho hayo, kuondoa mchoro huo. ANC kilisema mchoro wenyewe ni kumvunjia heshima rais na pia unakera. Hata hivyo wenye maonyesho wanasema kuwa kazi yao inalindwa na katiba ambayo inaruhusu watu haki ya kujielezea.
No comments:
Post a Comment