MCHEZAJI WA SIMBA PATRICKI MAFISANGO AFARIKI DUNIA
KIUNGO mkabaji wa kimataifa aliyekuwa akiichezea timu ya Simba Sports Club ya Jijini Dar es Salaam, Raia wa Rwanda, Patrick Mutesa Mafisango, amefariki dunia alfajiri ya leo kwa ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Tazara, Dar es Salaam.
Mafisango amekutwa na umauti huo wakati akiwa njiani kurejea nyumbani kwake, akitoka kujirusha na kwa sasa mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mafisango aliyejiunga na Klabu ya Simba akitokea timu ya Azam Fc, mwaka jana alizaliwa Machi 7, mwaka 1987, nchini Rwanda na kabla ya kutua nchini aliwahi kuichezea timu ya APR ya Rwanda.
Mchezaji huyo atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika Klabu hiyo kwa msimu huu uliomalizika hivi juzi na kung'aa zaidi katika Ligi hiyo kwa kupachika mabao na kutoa pasi za mwisho, ambapo Mechi ya mwisho ya Mafisango ilikuwa ni kati ya Simba dhidi ya Al Ahly Shandy Jumapili katika hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho, ambayo Simba ilitolewa kwa penalti 9-8, kufuatia sare ya jumla ya 3-3.
Wakati mechi ya kwanza kati ya Simba na Wasudan hao iliyochezwa hapa nyumbani katika Uwanja wa Taifa, Mafisango aliweza kuifungia timu yake bao moja kati ya matatu yaliyoiwezesha Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo huo.
Poleni wana Simba, Wanamichezo na Watanzania wote kwa ujumla, Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe.
AMINA.

No comments:
Post a Comment