Wednesday, May 23, 2012


MAPOKEZI YA MWENGE IRINGA MJINI YALIKUWAJE?

Wakati wa mapokezi ya mwenge huo katika eneo la Shule ya sekondari Tagamenda mjini Iringa.

Mahongo alisema kuwa Kati ya fedha hizo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imechangia kiasi cha shilingi milioni 25,503,397 wakati kiasi cha shilingi milioni 24,052,740 zimetokana na ruzuku na wananchi wa Manispaa ya Iringa wamechangia miradi hiyo jumla ya shilingi milioni 19,228,675 huku wahisani wamechangia kiasi cha shilingi milioni 144,709,300

Hata hivyo mkurungezi Mahongo alisema kuwa ushiriki wa wananchi wa Manispaa ya Iringa katika shughuli za kimaendeleo umeendelea kukua zaidi na kuwaomba wananchi kuendelea kuongeza kasi katika uchangiaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao.

Aliitaka miradi iliyopitiwa na mbio hizo za mwenge kuwa ujenzi wa ofisi ya kisasa ya mtendaji Kati ya Makorongoni mradi uliotumia kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 17.1 Kati ya fedha hizo wananchi wamechangia shilingi 500,000, mradi wa gulio la Kitwiru mradi uliotumia kiasi cha shilingi milioni 68,109,280.30 ,mradi wa vijana wa ufugaji nyuki na uhifadhi wa mlima Mkimbizi ambao imefikia kiasi cha shilingi milioni 22 fedha zilizotolewa na Halmashauri hiyo.

Mahongo aliitaja miradi mingine kuwa ni mradi wa SACCOS ya Rufiji Basin ambayo imeanzishwa kwa mtaji wa shilingi milioni 7.7 ,mradi wa ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari Kleruu ujenzi uliotumia kiasi cha shilingi milioni 8.9,mradi wa bweni katika shule ya sekondari Tagamenda uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 73.6 na miradi mingine mingi.

Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa ,kepten Mwanossa mbali ya kuipongeza Halmashauri hiyo ya Manispaa ya Iringa kwa kuibua miradi mizuri ya kimaendeleo bado aliwataka wananchi wanaozunguka miradi hiyo kuendelea kuitunza zaidi badala ya kuifanyia hujuma mbali mbali .

Kwani alisema lengo la serikali kutoa fedha hizo kwa ajili ya miradi ni kutaka wananchi kuendelea kunufaika na miradi hiyo na kutaka kasi hiyo ya wananchi kuchangia maendeleo kuendelea zaidi.

wakati huo huo kiongozi huyo wa mbio za mwenge Kitaifa Kepten Mwanossa ameonya tabia ya wanasiasa ambao wamekuwa wakibeza mbio hizo za mwenge wa Uhuru na kudai kuwa mwenge huo ni mwenge wa serikali na haufunfamani na Chama chochote cha kisiasa .

MWISHO

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...