Tuesday, March 20, 2012

GURUMO ANAENDELEA VIZURI HOSPITAL



Mwanamuziki mkongwe nchini wa bendi ya Msondo Ngoma,Muhidin Gurumo, akipatiwa huduma ya matibabu na muuguzi wa Hspitali ya Taif Muhimbili, Suraiya Mohamed, akiwa katika Hospitali hiyo leo jijini Dar es Salaam leo, ambako amelazwa toka wiki iliyopita kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kina kuhusu afya yake. Leo Gurumo alikuwa akipimwa mapigo ya moyo.


MWANAMUZIKI 
Mkongwe wa bendi kongwe ya muziki ya Msondo ngoma, Muhidin Gurumo aliyelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ugojwa wa shinikizo la damu anaendelea vizuri.
Akizungumza na mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, Hospitalini hapo leo, Msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila'Super 'D' alisema Afya ya Gurumo inaendelea vizuri na wakati wowote anaweza kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo na kurudi jukwaani.
Super D alisema kuwa madaktari wanataka kuchukua vipimo vya mwisho kwa kina kujua kila kitu kinachomsumbua katika mwili wake.

"Kwa sasa tunashukuru Mungu afya ya Gurumo inaendelea vizuri tofauti
na mara ya kwanza na akiendelea hivi anaweza hakurusiwa hivi
karibuni"alisema Super D.
Aidha Super D, aliwataka mashabiki wa bendi hiyo kumuombea duwa mwanamziki huyo ili apone upesi na kurejea jukwaani kuwapa burudani.

Alitaja ratiba ya bendi hiyo ya wiki hii kuwa ni:-
Alhamisi watakuwa Mwandege Mkoa wa Pwani,Ijumaa
watapiga katika viwanja vya Lidaz Clab jumamosi watakuwa katika
viwanja vya TCC Sigara na Jumapili watamalizia wiki endi yao katika ukumbi
wa Max Bar uliopo Ilala Bungoni.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...