Monday, March 26, 2012

FANALI YA MSHINDI DROO KUBWA YA MZUKA WA AIRTEL AKABIDHIWA ZAWADI YAKE MIL. 50 MKOANI MBEYA


Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania akimkabidhi bw Peter Lucas Laizer ambae ni mkazi wa Dodoma mfano wa hundi ya shilingi milioni 50 ikiwa ni zawadi yake aliyojishindia wakati wa droo ya mwisho ya promosheni ya MZUKA wa Airtel iliyosha hivi karibuni. Katikati anaeshudia ni ofisa huduma kwa wateja mkoa wa Mbeya  Bw Hamfrey George. Airtel imekabidhi mfano wa hundi hiyo mwishoni mwa wiki kwa dhamira ya kujulisha wateja wake tayari mshindi huyo ameshawekewa hela zakekatika akaunti yake




...Akishangaa cheki yake


Kutoka kulia na kushoto ni Ofisa huduma kwa wateja wa Airtel mkoani mbeya Hamfrey George na Giliadi Mshana wakimpongeza kwa namna ya kipekee bw Peter Lucas Laizer ambae ni mkazi wa Dodoma na pia mshindi wa droo ya kubwa ya mzuka wa airtel aliyejishindia shilingi milioni 50 za Airtel. Hafla ya makabidhiano ilifanyika  mwishoni mwa wiki mkoani mbeya ambapo mshindi huyo yuko huko kikazi na Airtel ilifanya hivyo kwa dhamira ya kujulisha wateja wake wote kuwa tayari mshindi huyo ameshawekewa hela zakekatika akaunti yake




Mwanahabari wa mkoani mbeya ambaye pia ni mmiliki wa blog ya Mbeya yetu Bw Joseph Misango akimpongeza  Peter Lucas Laizer mshindi wa droo kubwa ya mzuka wa airtel aliyejishindia shilingi milioni 50 za Airtel. Hafla ya makabidhiano ilifanyika  mwishoni mwa wiki mkoani mbeya ambapo mshindi huyo yuko huko kikazi



 Peter Lucas Laizer mkazi wa Dodoma na mshindi wa droo ya kubwa ya mzuka wa airtel aliyejishindia shilingi milioni 50 za Airtel akiongea na wanahabari mkani mbeya wakati wa hafla ya kukabidhiwa zawadi yake mwishoni mwa wiki. Hafla ya makabidhiano ilifanyika  mwishoni mwa wiki mkoani mbeya ambapo mshindi huyo yuko huko kikazi

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...