Monday, February 13, 2012



SIKIA HII…ASHA BARAKA KAA CHONJO....... TWANGA INAKUFA!!!





LEO napenda kupitia uzi huu kumpasha dada yangu IRON LADY, NIMESIKITISHWA SANA NA MWENENDO WA TWANGA. mimi ni mdau mkubwa sana wa muziki wa dansi haswaa bendi ya wabongo wenzetu ya twanga! baada ya mizunguko yangu wkendi hii Ijumaa tarehe 10 / 2 niliwasaka twanga nikawapata ndani ya RUFITA NIGHT CLUB NA KATI YA SEGEREA. ASHA NILICHOKIONA SIO KIZURI...... DAH NYIMBO MBILI TU, MTU PESA NA MWANA DSM NDIZO ZINANYANYUA WATU VITINI...USAFI BINAFSI WA WANAMUZIKI NI OVYO... VILE VIFULANA VYEUPE VYA WANENGUAJI WA KIUME VICHAFUUUU VYA BEI CHEEEE!!UGOMVI JUKWAANI HAKUNA MPANGILIO MZURI YAANI HAKUNA KIONGOZI ANAYEWAMASTA KILA MTU MBISHI... NILISHUHUDIA KWA MACHO YANGU SALEHE KUPAZA AKIMTAKA MPIGA GITA KUJA JUKWAANI KUPIGA GITA SAMBAMBA NA WENZAKE AKAMGOMEA WAKATUPIANA MANENO THEN AKAENDA KUSHTAKI KWA LWIZA NAE AKAMPTEZEA KUPAZA.... NILIUMIA SANA... YULE MPIGA GITA AKAWA HAPIGI GITA WAKATI KUPAZA ANAPOFIKIA KUIMBA HASA ULE WIMBO WA MWANAMKE MDANGANYIFU!!!!ULIMBUKENI WA SIMU JUKWAANI BAADHI YA WASANII WALIKUA KITUKO ZAIDI KWA KUFANYA VITU VIWILI KWA WAKATI HUKU ANAIMBA HUKU ANACHATI NA SIMU.... MNOGAAAA.... HII KUTU SIYO JAMANI.BIAAAA MAJUKWAAAANI....... ULEVI NOUMAAAAAHAKUNA REPA WA KUTISHAAA.... MRUDISHE FERGUSON KWA GHARAMA YOYOTE MI NAKWAMBIA YULE NI NOMA ANATHAMANI KUBWA KULIKO WANAMUZIKI WA KAWAIDA WA3 ULIONAO PALE. DOGO RAMA + WA BSS = FERGUSON. ACHA UBAHIRI MAMA. SISI BADO TUNAITAKA TWANGA.ACHANA NA WANAMUZIKI WA BEI CHEE TUMIA HELA UPATE HELA ... UKITAKA KULA SHARTI ULIWE DADA YANGU....NINAIPENDA SANA TWANGA.



Mwingine alishadadia hivi…

Usemayo ni kweli..

Mimi nilihudhuria kule ukumbi fulani maeneo ya Yombo hivi, kama unapitia Jet hivi..



Wako disorganized,na baadhi ya wanamuziki hawaji kwenye onesho,ama baadhi ya maonesho.....hata hivyo marekebisho madogo yanatakiwa,kwani la Twanga bado kubwa…

SIYO MANENO YA MATEJA20, NI MASHABIKI WA TWANGA NA HABARI KAMILI NI KWA MSAADA WA JAMIIFORUM

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...