Monday, February 6, 2012


MASHABIKI WAWADATISHA JUMA NATURE, NAMELES DAR LIVE




Msanii kutoka Kenya, Nameles akitumbuiza na mmoja wa mashabiki aliyeamua kumvunjia ukimya na kumpandia stejini baada ya kumuita.

Mashabiki waliofurika katika tamasha la Mwisho wa Mwezi lililofanyika usiku  wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa kijanja wa Dar Live Mbagala Zakhem, Dar es Salaam, wamewadatisha Juma Kassim Kiroboto ‘Juma Nature’ na David Masenge ‘Nameles’ waliokuwa wakiangusha burudani ya kihistoria.

Wakiwa kwenye makamuzi yao, Nature na Nameles walisikika wakitoa kauli za kushukuru umati mkubwa uliyojitokeza kwenye onesho hilo na kusema hawakutegemea Mbagala kuwa na mashabiki wa burudani wengi kiasi hicho.

Shoo hiyo ilisindikizwa na Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, Mashauzi Classic Band, Wakali Dancers, Zuhura na wasanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya huku washiriki wa shindano la Cheza, Vaa Imba kama Rihanna wakitambulishwa kwa mara ya kwanza katika ukumbi huo.




Nameles akitumbuiza.






Ambwene Yesayah ‘AY’, akisalimia kisanii na mashabiki hao mara baada ya Nameles kumaliza kutumbuiza.





Kiongozi wa Mashauzi Classic Band, Aisha Ramadhan ‘Isha Mashauzi’, akinengua na mpiga gitaa wake.





Isha Mashauzi akiwajibika jukwaani.





Juma Nature akipeana tano na mashabiki zake kabla ya kuanza makamuzi.





Kundi zima la TMK Wanaume Halisi likiwajibika stejini.




Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Zuhura akipagawisha.





Isha Mashauzi akiwajibika.





Mshiriki wa shindano la Cheza, Vaa, Imba kama Rihanna akionyesha uwezo wake wakati wa utambulisho wao.





Mshiriki mwingine wa shindano hilo akionyesha uwezo binafsi.





Wasanii wa kundi la Wakali Dancers wakikamua wimbo wa Michael Jackson.





Wanenguaji wa Bendi ya FM Academia wakionyesha uwezo wa kukata nyonga.





Washiriki wa shindano la Cheza, Vaa, Imba kama Rihanna wakionyesha shoo yao.





Washiriki hao wakiwa kwenye pozi la pamoja.





Juma Nature akiongea na mashabiki wake.


Wanamuziki wa FM Academia wakiwajibika.






Mashabiki waliofurika katika tamasha hilo wakifuatilia burudani.




Hali halisi ya umati ulioingia ukumbini hapo.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...