Monday, January 23, 2012

MREMBO AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA BODA BODA, MBAGALA USIKU WA KUAMKIA LEO



Mwili wa marehemu ukiwa chini muda mfupi baada ya ajali hiyo kutokea.


MREMBO
mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamka mara moja, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akidaiwa alikuwa  akitoka kupata raha kwenye Bar moja iliyopo Mbagala Kizuwiana jijini Dar es Salaam, baada ya pikipiki aliyokuwa amepakiwa kugongwa kwa nyumba na gari aina ya Lava4 lenye namba za usajili T 170 BBD.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 7:30 usiku wa kuamkia leo na  mrembo  huyo kufariki hapohapo huku Dereva wa pikipiki iliyokuwa imembeba akikimbizwa katika hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi, huku dereva wa gari lililomgonga akidaiwa kulitelekeza gari lake na kutokomea kusikojulikana.





Baadhi ya sehemu za miguu ya marehe zilizoumia.




Baadhi ya wananchi wa maeneo hayo wakijaribu kuutambua mwili wa marehemu.




Pikipiki iliyokuwa imembeba marehemu ikiwa kwenye eneo la ajali.






Gari lililosababisha maafa likiwa pembeni ya Barabara baada ya kutelekezwa na Dreva.






Mwili wa marehemu ukiwa umefunukwa.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...