Thursday, January 19, 2012

H-BABA KUTOKA NA BANZA STONE WIKI HII

MKALI wa miondoko ya Potezapoteza nchini , Hamis Ramadhan ‘H-Baba’ jana aliweka wazi kuwa tayari amekamilisha Single yake mpya inayokwenda kwa jina la SINARAHA, Ngoma hiyo ameifanya na msanii wa muziki wa dansi Bongo, Ramadhan Masanja, ‘Banza Stone’.

Akizungumza na na Mateja20 juzikati, H-Baba, alisema kuwa kibao hicho ni miongoni mwa nyimbo zake kumi zitakazokamilisha albam yake mpya itakayokwenda kwa jina la ‘SHIKA HAPA ACHA HAPA’ atakayoiingiza sokoni machi mwaka huu.

H-Baba alikamilisha kwa kusema kuwa ngoma hiyo aliyoifanya na Banza Stone, ameirekodi kawenye Studio ya Allan Mapigo na tayari ameshakamilisha maandalizi ya kurekodi video ya wimbo huo. H-Baba alisema kuwa katika wimbo huo mashabiki wake watarajie kupata vitu tofauti ikiwa ni pamoja na staili mpya na midundo iliyo ‘shiba’ na sauti murua ya Banza Stone, aliyeonyesha uwezo wake katika wimbo huo.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...