Tuesday, January 24, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi, alipozindua Daraja la Mingumbi lililopo Kilwa, wakati akiwa kwenye ziara yake ya Mkoa wa Lindi juzi, Januari 22, 2012. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovic Mwananzila.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Daraja la Mingumbi lililopo Wilaya ya Kilwa, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya Mkoa wa Lindi juzi Januari 22, 2012. Kushoto ni mkewe, Mama Zakhia Bilal (kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovic Mwananzila.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na mkewe Mama Zakhia Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovic Mwananzila na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Lindi, wakati akikagua Daraja la Mingumbi baada ya kuzindua daraja hilo lililopo Kilwa, akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya mkoa wa Lindi juzi, Januari 22, 2012.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwasalimia wananchi baada ya kuweka Jiwe la Msingi katika jengo la Kituo cha Afya cha Kitomanga lililopo Lindi Vijijini wakati akiwa katika zaiara yake mkoa wa Lindi juzi, Januari 22, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Msimamizi wa kituo cha afya cha Kitomanga, Dkt. Issa Michenje, kuhusu jengo jipya la Kituo cha afya cha Kitomanga, Lindi Vijijini, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi juzi Januari 22, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Jengo jipya la Bwalo la Shule ya Sekondari ya wasichana Ilulu, iliyopo Kilwa, wakati  akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya mkoa wa Lindi juzi, Januari 22, 2012. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovic Mwananzila.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea maeneo ya Shule ya Sekondari ya Ilulu, wakati alipofika shuleni hapo kwa ajili ya kuzindua Jengo jipya la Bwalo la Shule ya Sekondari ya wasichana, Ilulu, iliyopo Kilwa, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya mkoa wa Lindi juzi, Januari 22, 2012.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka jilwe la msingi katika Ofisi mpya ya Chama cha Mapinduzi CCM, iliyopo Chumo Namkamba Kilwa juzi, Januari 22, 2012, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya mkoa wa Lindi. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Chumo Namkamba, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi juzi, Januari 22, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikagua ujenzi wa jengo la Zahanati ya Kilanjelanje iliyopo Jimbo la Kilwa Kusini, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya Mkoa wa Lindi juzi, Januari 22, 2012.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...