Friday, August 2, 2013

MKE WA DR. SLAA AZUA TIMBWILI MAHAKAMANI....

JOSEPHINE Mushumbusi, mke wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa, jana alisababisha vicheko mahakamani baada ya kushindwa kumtambua mshtakiwa anayedaiwa kumpora maeneo ya SUMA JKT.

Josephine alimuacha mshtakiwam katika kesi yake na kumtambulisha mshitakiwa wa kesi nyingine kuwa ni miongoni wa watuhumiwa waliomvamia.

Hayo yalitokea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Riwa alipokuwa akitoa ushahidi kwa kuongozwa na Wakili wa Serikali Leonard Chalo.

Washitakiwa katika kesi hiyo ambao wanakabiliwa na shtaka la unyang'anyi wa kutumia silaha ni Getisi Mturi, Gake Mwita, Salum Mpanda na Charles Chasens.

Mturi na wenzake wanadaiwa Julai 13, 2011, eneo la Suma JKT makutano ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi, walimvamia Josephine na kumpora vitu mbalimbali na kabla ya kufanya uhalifu huo walimtishia kwa silaha.

Josephine alidai Julai 13 mwaka 2011, aliingia ofisini kwake katika jengo la Mawasiliano Tower saa 2.00 asubuhi na kutoka saa 11.00 jioni kwenda nyumbani kwake eneo la Boko akiendesha gari aina ya Toyota Harrier.

Alidai akiwa eneo la tukio katika foleni alimwona mtu akipita mkono wa kushoto huku akimuangalia kwa kutumia kioo cha pembezoni na ghafla alimuona akivunja kioo cha gari lake
Josephine aliidai alipoanza kuvunja dirisha alitahamaki lakini alisikia risasi hivyo aliamua kutafuta jinsi ya kujiokoa kwa kutoa gari eneo hilo na kwenda katika geti lililopo karibu na Suma JKT.
“Nilifanikiwa kuona sura ya mtu aliyenivamia kwa kuwa tulisimama wote kwa takribani dakika nane,”alidai Josephine.

Josephine alidai katika tukio hilo anakumbuka kulikuwa na watu si chini ya sita na walimwibia vitu mbalimbali. Kesi hiyo imepangwa kuendelea kusikilizwa Agosti 7 mwaka huu

NAY WA MITEGO AMPA MAKAVU ZITTO KABWE....AMTAKA AACHANE NA BONGO FLEVA NA BADALA YAKE AFANYE SIASA



Mfalme wa kudiss Tanzania, Nay wa Mitego amerejea tena kuchafua hali ya hewa kwa kutengeneza mijadala kwenye radio na kwenye mtandao kwa ngoma yake mpya, Salam Zao.
Kwenye Salam Zao, Nay ameendeela kufanya kile akifanyacho kwa uzuri (do what he does best) kuponda.
Awamu hii list ya aliowadiss imeongezeka zaidi na kuingia pia kwenye siasa huku akiendelea kuwapa madongo wana hip hop wenzie.

Ameanza kwa kumdiss Madee kwa kusema kuwa yeye ndio rais wa Manzese na kwamba Madee amesanda. “Mi ndo rais wa Manzese yule tozi kasanda, Manzese mikono juu naiongoza kamanda,” anachana Nay.
Nay wa Mitego ameendelea kuwadiss wana hip hip huku akiijita kuwa yeye ndio gangster rapper na anatengeneza hela huku wengine wakinuka vikwapa. Hakusita pia kuwarushia bombshell Weusi. “Yo Mchomvu wape salam ‘Kubumkubum’ waimbie watakufa njaa muziki umebadilika,” anarap Nay.

Nay pia amemdiss Zitto Kabwe kwa kurap:


“Word up Diamond, mwanangu wewe si mtoto wa Kigoma, mpe salama Zitto Kabwe mwambie afanye siasa aachane na Bongo Flava huku hatumtaki kabisa, maneno mengi, propaganda hajui kutekeleza, Kigoma Allstars tayari kawatelekeza.”

Rapper huyo pia amerap kuwa wapo watu waliojipatia utajiri kutokana na misiba ya Mangwea na Kanumba.

“Wanamiliki gari, wameota na vitambi kwa hela za rambirambi, mkizingua nawataja,”anasisitiza. Anasema tangu kifo cha Kanumba Bongo Movies imekufa na haiuzi tena.

Pia hajamuacha mwanzilishi wa shindano la Bongo Star Search Rita Paulsen kwa kudai kuwa licha ya kuwapa zawadi kubwa washindi, wameendelea kupigika mtaani.

“Hizi Salam ziende kwa madam Rita na Bongo Star Search. Mshindi analipwa nini mbona kama magumashi?! Namuona Walter Chilambo kapigika kama zamani, Haji Ramadhani kachoka yupo kitaani. Nauliza milioni hamsini zao anazila nani, acheni ubabaishaji wekeni mambo hadharani.”

Thursday, August 1, 2013

MWALIMU MKUU WA SHULE YA CHALINZE AHAMISHIA OFISI YAKE CHOONI....



MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Chalinze Mzee, wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, Elias Kapama, yuko katika wakati mgumu baada ya kuhamishia ofisi yake kwenye vyoo vya wanafunzi kutokana na jengo la ofisi yake kuharibika vibaya.

Hatua ya kuhamia chooni ilitokana na mkuu huyo kutawaliwa na hofu ya ubovu wa ofisi yake, hivyo kushindwa kufanya kazi zake kwa ufasaha unapotokea upepo au mvua.

Novemba 2012, Kapama alihamishia ofisi yake katika jengo la vyoo vya wanafunzi ambavyo havijaanza kutumika tangu ujenzi wake ukamilike mwaka 2011.

Akizungumzia hali hiyo, Kapama alisema kuwa anajisikia vibaya kutumia chumba maalumu cha kubadilishia nguo cha wavulana katika choo hicho kutokana na kukosa msaada kutoka halmashauri ya wilaya hiyo.

Alisema kuwa ni miezi tisa sasa tangu ahamishie ofisi yake chooni na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na ngazi ya wilaya pamoja na kufahamu mazingira hayo, hali aliyodai kuwa inamweka katika wakati mgumu.

“Sina ofisi, nimelazimika kuomba kwa wafadhili waliotujengea vyoo kwa ajili ya wanafunzi niweze kutumia chumba hiki cha kubadilishia nguo kama ofisi yangu hadi pale tutakapojenga ama kufanyia ukarabati ofisi ya zamani,” alisema.

Vyoo hivyo ambavyo vimejengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya Ebenezer Spritual Center ya mjini Chalinze, vimegharimu kiasi cha sh milioni 70 hadi kukamilika.

Mkuu huyo aliongeza kuwa kwa sasa walimu wanatumia tundu moja la choo huku wanafunzi 450 wakitumia matundu saba, matatu kwa wanawake na manne kwa wavulana.

Hata hivyo mwandishi wetu alishuhudia choo hicho kinachotumika sasa kikiwa hakina hadhi na usalama kwa watumiaji.

Aliuomba uongozi wa wilaya pamoja na wizara ambao umetembelea shule hiyo na kushuhudia mazingira hayo magumu kufanyia utekelezaji wa ujenzi wa ofisi hiyo haraka ili aweze kuhama kutoka chooni.

WAKATI SHEIKH PONDA AKITANGAZA KUGOMBEA URAIS, POLISI YATANGAZA KUMKAMATA KWA KUFANYA MIHADAHARA YA UCHOCHEZI



CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar kimemtuhumu Mwenyekiti wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, kuwa anaendesha kampeni za uchochezi wa kidini.

Uchochezi huo umedaiwa kuhatarisha amani ya nchi, hivyo kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kumchukulia hatua za kisheria.

Katibu wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu (NEC) Zanzibar, Itikadi na Uenezi, Waride Bakari Jabu, alisema jana kuwa ni wiki moja sasa tangu Ponda afanye mihadhara kwenye misikiti ya Mbuyuni, Kwarara na Nungwi kisiwani Unguja.

Waride alisema kuwa hotuba za Sheikh Ponda alizozitoa kwa nyakati tofauti kwenye misikiti hiyo zinapandikiza mbegu ya chuki, kuondosha upendo na kuhatarisha amani.

Alisema matamshi yake ni hatarishi kwa amani na utulivu uliopo, kwani anawataka Waislamu kupigana vita ya dini (Jihad) na kushiriki harakati za kuikomboa Zanzibar, kwa madai kuwa serikali iliyoko madarakani inawakandamiza na kuwanyanyasa wananchi.

“Sheikh Ponda ni hatari, anapanda shari na chuki miongoni mwa wananchi, anahamasisha wananchi wafanye uasi, kulipiza visiasi na kutaka waingie barabarani kwa maanadano ya kutetea haki kama inavyotokea Misri,” alisema.

Aidha, alisema CCM imeshangazwa na ukimya wa vyombo vya ulinzi na usalama wa raia kumtazama kiongozi huyo bila ya kumchukulia hatua za kisheria wakati akiwatukana matusi ya nguoni viongozi wa serikali na chama tawala.

Aliongeza kuwa Sheikh Ponda huenda anatumiwa na mtandao wa vurugu ili kuharibu na kuvuruga amani ambapo hamu yake ni kuona damu ya wananchi ikimwagika na nchi ikiingia kwenye machafuko.

Kwa mujibu wa Waride, kitendo cha Ponda kulitumia jukwaa la dini na kufanya siasa misikitini hakikubaliki na kwamba kikiachiwa kiendelee kinaweza kuleta madhara na mgawanyiko.

Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, alisema jeshi hilo limeanza kumtafuta Sheikh Ponda tangu walipopokea taarifa za kuendesha mihadhara ya uchochezi katika baadhi ya misikiti, ikiwa na lengo la kuibua chuki.

Mussa alisema kitendo anachokifanya kinakwenda kinyume cha sheria, hivyo kumtaka popote alipo ajisalimishe kwa hiari yake.

Tangu kuingia visiwani Zanzibar, Sheikh Ponda amekuwa akifungamana na viongozi wa Jumuiya ya Uamsho wakipinga kitendo cha viongozi wa jumuiya hiyo kuendelea kubakia mahabusu baada ya kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uharibifu wa mali na kuhatarisha usalama wa taifa.


Viongozi hao wa Uamsho wako mahabusu baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar, Ibrahim Mzee Ibrahim, kuwasilisha ombi la kufunga dhamana yao kwa kutumia sheria ya Usalama wa Taifa na marekebisho yake ya mwaka 2002

CHUMBA ALICHOPELEKWA ROSE NDAUKA CHAKUTWA NA KONDOMU TANO ZILIZOTUMIKA




Chumba cha hoteli ambacho Rose Ndauka alinaswa akiingia na dogo Nasry ambaye ni msanii wa bongo fleva, kimekutwa na kondomu tano zilizotumia...

Rose Ndauka ambaye ni mchumba wa Malik Bandawe,wiki iliyopita alinaswa akiingizwa katika chuba hicho na msanii Nassoro Ayoub "Nasry".

Kwa msaada wa wafanya usafi wa hoteli hiyo iliyoko maeneo ya kinondoni jijini Dar,wawili hao waliingia katika chumba namba G17 cha hoteli hiyo na kutumia masaa takribani matatu huku chumba kikiwa kimefungwa na walipotoka chumba kilikuwa hoi bin taaban....

"Mimi ndiye niliyefanya usafi chumba namba G17 siku hiyo na nilikuta kondomu tano zilizotumika huku shuka zikiwa zimevurugika kabisa."..Alifunguka mfanya usafi huyo

Tukio la binti huyu kunaswa akiingizwa hotelini na dogo Nasry linatia shaka uchumba wake na Malik Bandawe ambaye kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitangaza mipango yao ya kufunga ndoa

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...