Saturday, August 8, 2015
Monday, August 3, 2015
Nuh Mziwanda amuomba penzi Wema!
Musa Mateja
YELEUWIII! Katika hali ya kushangaza, sauti ya mpenzi wa staa wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ inayosikika akimtongoza Wema Sepetu imemfikia Shilole na kusababisha azimie, Ijumaa Wikienda linakupa ‘ubuyu’ kamili.
BETHIDEI YA SHAMSA Tukio hilo lililozua mtafaruku lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar kulipokuwa na pati ya bethidei ya mwigizaji Shamsa Ford.
TUJIUNGE NA CHANZO Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho kilishuhudia tukio hilo mwanzo-mwisho, saa chache baada ya kumalizika kwa shughuli ya kulishana keki, waalikwa walishangaa kumuona Shilole akiishiwa nguvu na kudondoka baada ya kusikiliza ujumbe wa sauti aliotumiwa kwenye simu.“We acha tu. Ilikuwa balaa. Watu tulikuwa katika shamrashamra ya kulishana keki, ghafla tukashangaa mwenzetu anaishiwa nguvu na kuanguka,” kilieleza chanzo.
Staa wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, akiwa na mpenzi wake wa sasa Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’.
SHILOLE AMFUATA NUH Chanzo hicho kilieleza kuwa, baada ya kuusikiliza ujumbe huo, Shilole alimfuata Nuh kwa ajili ya kumsikilizisha lakini Nuh alijibu ‘mbovu’ ndipo Shilole alipomuomba ufunguo wa gari waliyokwenda nayo, akarudi alipokuwa amekaa awali.
APOTEZA ‘NETIWEKI’ “Aliporudi alipokuwa amekaa, Shilole alijikuta akiishiwa nguvu na kuzimia ambapo Aunt Ezekiel na kina JB (Jacob Stephen) walipofanya kazi ya ziada kumpepea, huku wengine wakihangaika kummwagia maji kunusuru afya yake. “Walifanikiwa kumpandisha kwenye gari lake. Joto lilikuwa kubwa kufuatia hali hiyo maana kila mtu alishindwa kuelewa kilichotokea, hivyo Shilole, baada ya kuzinduka aliulizwa kilichomfanya azime ambapo aliwasikilizisha sauti hiyo kila mmoja akabaki ameduwaa,” kilieleza chanzo.
AUNT AOKOA JAHAZI
Ilielezwa kuwa, mwigizaji Aunt Ezekiel ndiye aliyeokoa jahazi kwa kulazimika kuendesha gari la Shilole na kumpeleka nyumbani huku Nuh akipandishwa kwenye gari la JB kumpeleka kwa ndugu zake.
MSIKIE SHILOLE Paparazi wetu, baada ya kupenyezewa ubuyu huo, alimtafuta Shilole ili kupata habari kamili ambapo alikiri kupokea ujumbe huo wa sauti huku akiainisha kuwa umemkera kwani kuna maneno yanasikika akimponda yeye. “Inaniuma sana, Nuh kuendelea kunidhalilisha kiasi hicho wakati ni mwanaume ambaye ninamheshimu, tunakoelekea uzalendo utanishinda.
“Nilipousikiliza ujumbe ule kwa mara ya kwanza sikuamini nilichokisikia. Pamoja na Wema kuonesha wazi msimamo wa kumkataa Nuh ila mimi naona kama fedheha kubwa kwangu kwani ninamheshimu sana. “Watu wananiona mimi mkorofi lakini kama ningekuwa napenda kuweka kila jambo wazi, hakuna mtu angeendelea kunifikiria vibaya.“Siwezi tena kuendelea kuumiza moyo wangu kila kukicha,” alisema Shilole ambaye anatumikia kifungo cha Basata kwa kutojishughulisha na sanaa kwa takriban mwaka mmoja kwa kosa la kucheza nusu utupu jukwaani.
Diamond Platnumz ameshinda tuzo zingine mbili
FAVOURITE SONG OF THE YEAR (Nana)
FAVOURITE ARTIST OF THE YEAR
thanks alot @Africannafca

(Naomba nitumie Muda huu kuwashkuru Mashabiki zangu wote kwa Mapenzi na Sapoti yenu ya Dhati mnayoendelea kunipa…ningependa niwataarifu kuwa kijana wenu mmeniwezesha kushinda tunzo mbili ambazo ni MSANII ANAEPENDWA AFRICA na NYIMBO INAYOPENDWA AFRICA (#NaNa ) kwenye Tunzo za NollyWood & African people Choice Awards @Africannafca zitazotolewa tareh 12 /09 /2015

