Wednesday, June 10, 2015

SHAMSA AWAKANDIA MABWANA ZAKE

STAA wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford ameibuka na kuwakandia mabwana aliowahi kutoka nao kimapenzi na kusema kuwa ni wababaishaji na sasa ni bora atafute mwanaume wa kumuoa.
Staa wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford.
Akipiga stori na Amani, Shamsa anayetikisa na Filamu ya Chausiku alisema, kwa sasa amejipanga kuolewa wakati wowote iwapo tu mwanaume mwenye sifa anazozitaka atajitokeza.
“Wengi niliowahi kuwa nao ni wababaishaji tu na wala sikuona mwanaume wa kuweza kunioa. Kwa sasa nimeshakua mtu mzima na ikitokea wa kunioa nipo tayari,” alisema Shamsa.
Awali Shamsa alikuwa akitoka na mtu aliyetambulika kama Dick na kupata naye mtoto mmoja, baada ya hapo ilidaiwa bidada huyo kaingia kwenye uhusiano na Nay wa Mitego.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...