Thursday, June 11, 2015

NAY, PAM D WAGANDANA KIMAHABA

YA leo siyo ya kesho! Wakati Juni 9, mwaka jana, nyota wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki  ‘Nay wa Mitego’ alisherehekea siku ya kuzaliwa kwake ‘bethidei’ kwa mbwembwe kubwa ambayo iliandaliwa na mzazi mwenzake, Siwema pale Kimara Barudi, Dar, mwaka huu ziii huku akinaswa kimahaba na Mbongo Fleva, Pamela Daffa ‘Pam D’.
Nyota wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki  ‘Nay wa Mitego’ akiwa na mbongo Fleva, Pamela Daffa ‘Pam D’ wakiwa kimahaba.
Jumanne iliyopita, Nay alijikuta akisherehekea siku hiyo bila kuwa na hekahaka ambapo mapaparazi wetu walimkuta kwenye Studio ya De Fetality ya Mensen Selekta iliyopo Sinza ya Madukani, Dar na baadaye alijikuta akiloweshwa maji na prodyuza wake, Tee Touch.
Kwa mujibu wa mfanyakazi mmoja ndani ya studio hiyo, Nay, jioni ya siku hiyo alikuwa kwa mama yake mzazi, Kimara akiwa anajua siku imepita na hakuna cha sherehe.
“Ilikuwa saa tatu usiku, Tee Touch akamuuliza aliko, akasema kwa mama yake, akamwita aje hapa kunna kazi ya kufanya. Kufika tukammwagia maji ya baridi tu kama kumpongeza kwa kuzaliwa kwake,” alisema mfanyakazi huyo.
Nay, akiwa katika hali ya kushangaa, mara alitokea Pam D anayetamba na singo yake ya Nimempata akiwa amevalia gauni jekundu la mtoko wa usiku na viatu vya mchuchumio kisha akamkumbatia Nay huku akisema:

“Happy birthday Nay wangu,” na kumsindikiza na mabusu mfulululizo ambapo waligandana kwa muda usiopungua dakika tatu huku wakioneshana meseji kwenye simu na kuzungumza mambo yao. Matukio yote hayo yalikuwa yakijiri nje ya studio hiyo.
Wakipozi kimahaba.
Tukio la Nay na Pam D kung’ngang’aniana kimahaba lilizua maswali na mshangao kwa baadhi ya wafanyakazi wengine wa studio hiyo wakitaka kujua kama ni wapenzi au la!
Baadaye mapaparazi wetu walimfuata Nay na kumuuliza swali la kwanza, kulikoni amwagiwe maji vile!

“Mimi nilijua wameniita kama siku nyingine ambapo huwa tunakutana kufanya kazi, nimeshangaa nafika wananimwagia maji. Tena wamenimwagia mpaka maziwa ya ng’ombe. Hapa nimeanza kuhisi vichomi,” alisema Nay.
Akaulizwa swali la pili, ni kwa nini Shamsa Ford, msanii anayetajwa kuwa naye kwa sasa hakuwepo!
“Mimi sijui. Mimi sikupanga kuwe na sherehe leo.”

Akaulizwa swali jingine kama yeye na Pam D ni wapenzi.
“Teh! Teh! Jamani! Jamani! Daaa!”

 
Akaulizwa anajisikiaje kutokuwepo kwa Siwema katika tukio hilo fupi kama ilivyokuwa mwaka jana!
“Hamna shida wala! Hamna shida kabisa. Haya mambo yapo tu.”

Mapaparazi wetu walimgeukia Pam D na kumuuliza kama kwa sasa amejiegesha kimapenzi kwa Nay!
“Nimekuja kum-wish happy birthday yake jamani. Kwani kuna tatizo? Namkubali sana Nay wangu. Si mnajua niko naye kwenye fani,” alisema Pam D na kumkumbatia tena Nay.

Juzi, Ijumaa liliwasiliana na Shamsa na kumuuliza kulikoni hakuonekana katika siku ya kuzaliwa ya Nay, alijibu:
“Nauguza, mama yangu anaumwa.”

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...