Saturday, June 20, 2015

KUMUONA MTOTO WA ZARI, MIL.20

AMA kweli Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Mama Kijacho, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, sasa ni wa kimataifa zaidi ambapo wakati mwanamama huyo akijiandaa kujifungua, tayari mtoto ajaye ameandaliwa chumba maalum cha kulala na gharama za kumuona kwa atakayehitaji picha hasa za kwenye vyombo vya habari, itakuwa si chini ya Sh. milioni 20.
Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Mama Kijacho, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
CHANZO KUTOKA WCB
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho kipo ndani ya Wasafi Classic Baby (WBC), Diamond na Zari wameamua kutenga chumba maalum cha mtoto wao atakapozaliwa.
Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akiwa katika pozi na lafiki yake.
MASHARTI YA KUMWAGA
Ilidaiwa kwamba, chumba hicho kitakuwa mahususi kwa mtoto tu na wala hakuna mtu mwingine atakaye ruhusiwa kuingia kumuona bila malipo zaidi ya mama, baba na familia yao ambao nao wataingia kwa sharti la kutopiga picha.

“Naona Zari anampeleka Diamond kimataifa kila kukicha maana nimeshuhudia chumba kina ‘full’ mazagazaga ya mtoto na nilipouliza nikaambiwa hicho ni chumba cha mtoto wa Zari mara tu atakapozaliwa.
“Wanasema mtoto atakuwa na chumba chake maalum na hataruhusiwa mtu mwingine kulala wala kumuona.
“Kwa watu wa media (vyombo vya habari) lazima watoe si chini ya milioni 20 kwa picha na interview (mahojiano) na Zari.
KAMA KANYE NA KIM
“Wameamua kufanya hivyo ili kuendana na wasanii wengine wa Marekani kama Kanye West na Kim Kardashian au Jay Z na Beyonce ambao wamekuwa wakifanya hivyo.
ULINZI USIPIME
“Nimeshuhudia hadi vitu vya mtoto na kitanda chake tayari vimeshaandaliwa mara tu mtoto atakapokuja atakuwa katika chumba hicho ambacho kipo ndani ya mjengo wao, Madale (Tegeta, Dar). Unaambiwa ulinzi utakuwa mkali usipime.
“Wamejipanga mtu yeyote asimuone mtoto huyo kuanzia siku anajifungua kwani wanategemea kuweka ulinzi wa hali ya juu kuanzia hospitalini hivyo hata wanahabari wakihitaji lolote juu ya mtoto huyo watatakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha,” kilitiririka chanzo hicho.
BABA KIJACHO ANASEMAJE?
Baada ya kunyetishiwa mchongo huo, gazeti hili lilimtafuta Baba Kijacho, Diamond ili kuthibitisha ishu hiyo ambapo alisema ni kweli wameshaandaa chumba maalum kwa ajili yake, mara tu atakapozaliwa na kwamba haitaonekana sura yake kwani kutakuwa na bei maalum kwa yoyote atakayehitaji kumuona.
“Yeah! Ni kweli kuna chumba chake maalum na pia haitaonekana sura yake maana kutakuwa na bei maalum kwa magazine au televisheni itakayohitaji kuwa na ‘exclusive’ ya kuonesha sura yake kwa mara ya kwanza.
“Bei ya mtu kumuona au kwa vyombo vya habari, hiyo itategemea na ukaribu wetu na chombo husika kitakachokuwa kikihitaji kurusha habari ya mtoto wetu,” alisema Diamond anayesumbua na kibao chake kipya cha Nana.
DIAMOND PRESHA TUPU
Diamond kwa sasa yupo kwenye presha kubwa ya kuomba mashabiki wake wampigie kura kwa wingi katika Tuzo za MTV (Mama’s) baada ya kuteuliwa kuwania Vipengele vya Msanii Bora wa Kiume Afrika, Mtumbuizaji Bora wa Kiume Afrika na Nyimbo Bora ya Kushirikiana Afrika.
ZARI ATAJIFUNGUA LINI?
Kwa upande wake, Zari anatarajiwa kujifungua mtoto wa kike kuanzia Agosti, mwaka huu na kuendelea.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...