Thursday, June 18, 2015

KARRUECHE, CHRIS BROWN WAFIKA PABAYA!


 
Mtangazaji na mwanamitindo, Karrueche Tran.
New York,Marekani
MTANGAZAJI na mwanamitindo, Karrueche Tran amemchana mpenzi wake wa zamani, Christopher Maurice ‘Chris Brown’ katika mitandao ya kijamii.
 
Karrueche Tran akiwa na aliyekuwa mpenzi wake, Christopher Maurice ‘Chris Brown’.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Karrueche alimfungukia Chris kuwa asimfuatefuate kwani mapenzi yao yalishakwisha tangu alipogundua kuwa amezaa na mwanamke mwingine.“
@chrisbrownofficial ulifanya mahojiano na Ryan Seacrest na ukaniongelea na ndiyo maana hata nilipofanyiwa mahojiano na Access Hollywood niliulizwa kuhusu wewe na nilijibu kama mtu aliyepevuka.“Niliongelea maisha yangu. Sikukuongelea. Usiwe mpumbavu wakati unajua uhusiano wetu ulikosa uaminifu.”

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...