Saturday, June 20, 2015

HARUSI YA BABA HAJI MASTAA WAFANYA KUFURU

SAA chache kabla ya kuanza kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, staa wa sinema za Kibongo, Haji Adam ‘Baba Haji’ ameangusha bonge la harusi baada kufunga ndoa na mrembo aliyetajwa kwa jina la Latifa Sharji wiki moja iliyopita huku mastaa wakifanya kufuru kama kawaida yao.
Staa wa sinema za Kibongo, Haji Adam ‘Baba Haji’ akivishwa pete na mkewe Latifa Sharji.
Kabla ya pati hiyo iliyochukua nafasi kwenye Ukumbi wa Escape One uliopo Mikocheni, Dar usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita, Baba Haji alifunga ndoa na Latifa katika Msikiti wa Bungoni, Ilala jijini Dar.
Katika pati hiyo iliyohudhuriwa na mastaa kibao wa Bongo Movies huku gazeti hili nalo likijipenyeza ndani, waalikwa walikula na kunywa hadi wakasaza kabla ya muda wa zawadi na kusakata muziki.Kwenye shughuli hiyo, kadiri watu walivyokuwa wakipiga ulabu ndivyo sherehe ilivyokuwa ikichangamka na mastaa kujikuta wakiserebuka muziki kwa kwenda mbele.
Jacqueline Wolper Massawe, akisakata rhumba.
Muda wa kutunza ulipowadia ndipo mastaa walipoanza kushindana kuwamwagia wanandoa hao ‘minoti ya wekundu wa msimbazi’.

Baadhi ya wasanii walioongoza kutunza ni tajiri mfupi, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ambaye alimwaga fedha taslimu Sh. milioni 2 akifuatiwa na Single Mtambalike ‘Richie’, Jacob Steven ‘JB’, Vincent Kigosi ‘Ray’ na wengine waliokuwa fedha za kudunduliza.
Kwa upande wa mastaa wa kike, Kajala Masanja ‘Kay’ aliongoza kwa kumwaga mkwanja akifuatiwa na Jacqueline Wolper Massawe, Wastara Juma, Jennifer Kyaka ‘Odama’, Lulu Mathias Semagongo ‘Anti Lulu’ na watoto wengine wa mjini.
Muda wa kuserebuka ulipofika ilikuwa ni balaa tupu kwani Wolper aliweka shida chini, akatupa mikono kule na kumwaga mauno hadi akajikuta akimwaga ‘lazi’.
Hadi gazeti hili linaanua jamvi ukumbini hapo usiku mnene, baadhi ya mastaa walikuwa wakiendelea kusakata rhumba na kupiga kinywaji.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...