Saturday, June 13, 2015

GLOBAL YAPATA PIGO

Marehemu Robert Ridochi Tilya enzi za uhai wake.
WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, watayarishaji wa magazeti ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi, wamepata pigo kwa kuondokewa na mfanyakazi mwenzao, Robert Ridochi Tilya aliyefariki alfajiri ya leo kwa ajali ya gari.
Robert alipata ajali hiyo maeneo ya External-Ubungo jijini Dar baada ya Lori kumbana na gari aina ya Toyota Noah alilokuwa akiendesha Robert kuingia kwenye mtaro na kufariki papohapo.
Kwenye gari alilokuwa akiendesha Robert, alikuwa amewapakiza abiria wawili ambao wamepata majeraha na wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa ya  Muhimbili.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
Mungu ailaze roho ya marehemu Robert mahali pema peponi-Amina.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...