Tuesday, April 14, 2015

PACQUIAO AJICHUA VIKALI KUELEKEA PAMBANO LAKE LA KARNE DHIDI YA MAYWEATHER


Manny Pacquiao akijiandaa na pambano lake dhidi ya Floyd Mayweather.
Maandalizi yakiwa yamepamba moto kwenye gym ya masumbwi ya Wild Card iliyopo Los Angeles nchini Marekani.
BONDIA mahiri kutoka Ufilipino, Manny Pacquiao ameendelea kujichua vikali katika gym ya masumbwi ya Wild Card iliyopo Los Angeles nchini Marekani.
Pacquiao anajiandaa na pambano lake kali dhidi ya Floyd Mayweather litakalopigwa Mei 2, mwaka huu katika Ukumbi wa MGM Grand Garden jijini Las Vegas, Marekani.
Pambano hilo linatazamiwa na wadau wa masumbwi kuwa la karne kutokana na umahiri wa mabondia hao wawili.
Pichani juu ni taswira mbalimbali za Manny Pacquiao akiwa mazoezini.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...