Tuesday, April 14, 2015

MAMA MZAZI WA BEYONCE, TINA AFUNGA NDOA YA PILI NA MSANII RICHARD LAWSON

Mama Beyonce, Tina akiwa na mumewe Richard Lawson siku ya ndoa yao juzi Jumapili.
Tina akiwa na mwanaye Beyonce mwaka 2013.
Kifamilia zaidi: Familia hii imekuwa na baraka baada ya mwaka jana Solange (wa kwanza kulia) kufunga ndoa na Alan Ferguson. Pichani ni Beyonce, Jay Z na Tina.
MAMA mzazi wa mwanamuziki Beyonce, Tina (61) amefunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi ambaye ni msanii Richard Lawson, mwenye umri wa miaka 67.
Tina na Richard walifunga pingu za maisha katika boti moja la kifahari karibu na ufukwe wa Newport California juzi Jumapili.
Tina akiwa na mumewe wa zamani, Mathew Knowles mwaka 2006.
Miongoni mwa waliohudhuria harusi hiyo ni pamoja na binti wa mama huyo, mwanamuziki Beyoncé na mumewe Jay Z pamoja na dada yake Beyonce, Solange Knowles.
Imekuwa ni msimu wa baraka kwa familia ya bi. Tina ambaye mwaka uliopita alishuhudia ndoa ya mwanaye Solange na promota wa muziki, Alan Ferguson.
Tina akiwa na mumewe wa sasa Richard mwaka jana.
Haijabainika iwapo baba yao mzazi akina Beyonce ambaye pia aliwahi kuwa meneja wa Beyonce' bwana Mathew Knowles alikuwepo.
Mathew, 63, aliishi na Tina kwa miaka 31 kati ya mwaka wa 1980 na 2011 na walijaaliwa watoto wawili Beyonce na Solange.
Mama na watoto wake: Tina (kulia) akiwa katika pozi na mabinti zake Solange na Beyonce.
Baada ya wawili hao kutofautiana Mathew alimuoa bi. Gena Charmaine mwaka wa 2013 huko Houston, Texas Marekani.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...