Wednesday, April 8, 2015

ALI CHOCKY ATUA RASMI TWANGA PEPETAKiongozi wa Twanga Pepeta, Luiza Mbutu (katikati) akiwatambulisha waimbaji Ali Chocky na Super Nyamwela.

Ali Chocky (kushoto) akiwa na Super Nywamwela wakizungumza na waandishi wa habari katika Hotel ya NEMAX Royal iliyopo Kinondoni baada ya kurudi Twanga Pepeta.ALIYEKUWA Mkurugenzi wa kundi la muziki la Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’, Ali Chocky, ameamua kurudi katika bendi yake ya zamani ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ inayomilikiwa na Asha Baraka ambaye ni mkurungezi wa bendi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Nemax Royal, kiongozi wa Twanga Pepeta, Luiza Mbutu,  amesema kurudi kwa wakongwe na waasisi kwenye bendi yao ambao ni Chocky na Super Nyamwela, kutaleta nguvu mpya na mapinduzi katika muziki wa dansi nchini kutokana na uwezo wao binafsi.
Kwa upande wake,  Chocky amesema kuamua kwake kurudi katika bendi yake ya zamani ni kutokana na mapenzi yake binafsi na wala hajalazimishwa na mtu huku akisisitiza kuwa hajafulia na ndiyo kwanza moto umeanza.
“Tupunguze maneno-maneno; kurudi kwangu na Super Nyamwela ndani ya Twanga si kitu cha ajabu, tumeamua wenyewe na kila mtu ana uhuru wake binafsi wa kufanya jambo kwa muda muafaka bila kupangiwa.
“Wakati nasafiri kwenda Japan niliwaambia wanamuziki wa bendi yangu kwamba yeyote anayeweza kunisubiri anisubiri na kama wapo watakaotaka kuondoka waende, lakini niliporudi niliwakuta wameshatawanyika, sasa nipo nyumbani.  Mashabiki wangu wategemee makubwa kutoka kwangu kwani muda si mrefu nitaanza kupakua nyimbo kama vile Kichwa Chini, Usiogope Maisha na nyingine nyingi,” alisema Chocky.
 

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...